Jumatano. 04 Desemba. 2024
feature-top
Matokeo ya upashaji joto wa sayari unaonekana kuporomoka kwa barafu hata upungufu wa maji kama vile Ziwa Chad Barani Afrika

Tarehe 25 Januari 2019 Askofu Mkuu Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York ametoa hotuba yake kuhusu majadiliano ya majanga ya tabia nchi, amani na usalama wa Kimataifa na kurudia kukazia wito wa Baba Mtakatifu Francisko kuhusiana na uongofu wa kiekolojia

Janga la matokeo ya tabia nchi katika nchi zote yanatoa msukumo wa kujikita katika juhudi za dharura kwa ngazi ya ulimwengu hasa kwa  ajili ya mataifa masikini, kwa sababu mchezo haupo katika maisha ya binadamu na rasilimali zake tu  lakini pia hata katika amani na usalama wa kimataifa. Ndiyo wito uliotolewa na Askofu Mkuu Bernadito Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York  Marekani wakati akitoa hotuba  yake  kuhusu majadiliano ya majanga ya tabia nchi, amani na usalama wa Kimataifa.

Sababu za mabadiliko ya tabia ncni na kuongezeka kwa migogoro

Matokeo ya upashaji joto wa sayari, unaanza tayari kuoneakana hasa katika nchi masikini zaidi, kwa wale ambao wanalipa gharama za kuonegeza kwa mabadiliko ya tamina nchi kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni. Askofu Mkuu Auza kwa kuthibitisha hayo, ametaja mojawapi kati ya nchi nyingi kama kesi ya Ziwa Chad ambapo upungufu wa maji wa kiasi kikubwa unaendeleza kusababisha wimbi la watu kuhamia ardhi yao yenye rotuna kwasababu ya kuongezea kwa migogoro, na ghasia za kigaidi.

Ili kuweza kuzuia matokeo hayo mengi yanayo sababisha na kuongezeka kwa joto katika nyumba ya pamoja, lakini pia hata kupunguza matokeo yake ya ukosefu wa amani na usalama duniani, Askofu Mkuu Auza anathibitisha ya kuwa inahitajika kujikita katika matendo ya dhati kwa haraka, kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na Ripoti ya mwisho ya Kikundi kisicho cha serikali cha wataalam wa mabadiliko ya Tabianchi (IPCC). Mambo ya dhati ni kama yale ya kuongeza nguvu serikali kwa ngazi zote ili kuboresha kwa dhati taasisi wahamasishaji na mbinu za kiteknoloja, kuongeza nguvu za kisiasa katika kuwekeza kwenye mabadiliko ya tabia nchi na kuruhusu mabadiliko ili kubadili mtindo wa maisha.

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika wote kuwa na uongofu wa kiekolojia

Matendo haya yote, Askofu Mkuu Auza anakumbusha ni yale ambayo ni sehemu ya uongofu wa kiekolojia kama alivyosisitiza Baba Mtakatifu Francisko na kuwaalika Jumuiya za Kimataifa na kila mtu kujikita katika uongofu huo. Hatimaye anakofu mkuu anatudia kutoa wito huo huo wa Baba Myakatifu wa kujikita kwa nguvu zote kwa sehemu zote za Mataifa, katika kuongeza nguvu ya ushirikiano, ili kupambania dharura yenye kuleta wasiwasili mkubwa wa matukio ya ongezeko la joto duniani.Kutokuwa na uwezo wa kufanya hivyo unatendelea kuwalazimisha waathirika wapambane kutafuta chakula na kuzuka kwa vita kwa ajili ya maji.


Maoni


Ingia utoe maoni