Watu 20 wamefariki dunia na majeruhi 81 katika chambulizi la kigaidi ndani na mbele ya Kanisa Kuu Katoliki la Mama Yetu wa Mlima Karmeli mjini Jolo, Kusini mwa nchi ya Ufilippini wakati wa madhimisho ya Misa Takatifu Jumapili tarehe 27 Januari 2019. Polisi wa kanda anathibitisha kuwa waathirika ni raia 15 na wanajeshi 5 huku wanajeshi 14, polisi wawili na raia 65 wamejeruhiwa. Kwa mujibu wa Mkuu wa Usalama anasema Mabomu mawili yalilipuka wakati raia wako wanasali Kanisani.
Bomu la kwanza kulipuka ni ndani ya Kanisa kuu na bomu jingine nje ya Kanisa mahali pa kuegesha magari, wakati vikosi vya usalama vimeanza operesheni ya kupambana na magaidi. Miili ya wathirika na waliojeruhiwa wamepelekwa hopitali karibu na mji wa Zamboanga. Shirika la Kipapa cha Kanisa hitaji linaomboleza na ndugu na jamaa wote wa waathirika wa mashambulizi hayo katika wilaya mko wa Mindanao .
Askofu Mstaafu Lito Lampone ameeleza katika Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji kuhusu mabomu hayo mawili yaliyotegwa ndani na nje ya Kanisa. Bomu la Kwanza lilipuka wakati watu wanaimba Aleluya na la pili wakati vikosi vya usalama wakipambana na magaidi.Naye msimamizi wa Kitume wa Jolo padre Romeo Saniel, wametoa salama za rambi rambi kwa sababu wakati wa shambuli , kama vile Askofu Lampon walikuwa katika Mkutano mkuu wa Mwaka huko Manila. Sehemu kubwa ya watu walioathirikia ni waamini ambao kila Jumapili walikuwa wanakwenda misa ya saa mbili asubuhi.
Askofu Saniel anathibitisha kuwa na uhakika kuwa shambulizi hili linatokana na kuteswa kwa wakristo na wathirika wote wameuwawa kwa sababu ya kutetea imani yao. Hii ni kutokana na kwamba hakuna maelezo mengi ya kusema kwani uchungu hivyo inatakiwa kusali kwa ajili ya waathirika wote na familia zao kama vile hata familia za wanajeshi waliopoteza maisha wakitafuta kuweka usalama wa Kanisa Kuu.
Maoni
Ingia utoe maoni