Alhamisi. 21 Novemba. 2024
feature-top
Papa akiwa Panama atakutana hata na vijana wafungwa gerezani, pia vijana walemavu na wenye ugonjwa wa ukimwi

Imeandikwa na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Pamoja na vijana wengi watakaoweza kukutana na Baba Mtakatifu Francisko huko Panama, wapo wengine atakaowatembelea katika Gereza la watoto, pia kituo cha vijana walemavu na wenye ugonjwa wa ukimwi, kwakuwa hawa hawatakuwa na fursa za kushiriki Siku ya vijana na wenzao. Hayo yamethibitishwa na Msemaji Mkuu wa habari Vatican, Bwana Gisotti

Mkutano na vijana katika magereza ya watoto wadogo itakuwa ndizo sura za vijana wa kwanza kumwona Baba Mtakatifu,pia mkutano mkutano mwingine wa vijana wagonjwa ambao watakutana na Baba Mtakatifu wakati wa Siku ya vijana duniani mjini Panama. Amethibitisha hayo Msemaji Mkuu wa mpito wa habari Vatican, Bwana Alessandro Gisotti, kufuatia na matukio mengine katika ratiba kati ya tarehe 25 na 27 Januari 2019.

Msemaji Mkuu wa Vatican kwa waandishi wa habari anathibitisha kuwa tarehe 25 Januari ni siku ambayo itajikita kufanya Njia ya Msalaba, ambapo Baba Mtakatifu ataondoka asubuhi kuelekea katika Gereza la watoto wadogo huko Las Garzas de Pacora, mahali ambapo atakutana na vijana wafungwa 200. Baba Mtakatifu anakwenda kukutana na vijana ambao hawawezi kuudhuria Siku ya Vijana na wenzao anasema Bwana Gisotti na kuongeza  kusema  kuwa, hii ni kwa mara ya kwanza katika Siku ya Vijana, kuweka liturujia ya kitubio ambayo itafanyika ndani ya magereza. Baadaye Baba Mtakatifu  wakati wa kuwatembelea vijana hao atawaungamisha baadhi ya wafungwa katika sanduku lililotengenezwa na badhi ya wafungwa hao vijana.

Aidha tarehe 27 Januari  ambayo ni siku ya mwisho ya Vijana, Bwana Gisotti amesema kuwa mara baada ya Misa Takatifu saa 2.00 asubuhi katika Uwanja wa mpira wa Mtakatifu Yohane Paulo II , uwanja wenye uwezo wa kuwa n anafasi za watu 700,000 Baba Mtakatifu atakwenda katika nyumba ya Hogar iitwayo Mchungaji Mwema, ili kukuta na vijana walemavu na wenye ugonjwa wa ukimwi katika lengo la kuonesha kweli umakini kwa wadhaifu na vijana wanaoteseka amesema Bwana Gisotti.

Ndege ya Kipapa huko Panama inatarajiwa kuwasiri uwanja wa ndege tarehe 23 Januari 2019 majira ya saa 10.30 za jioni na kupokelewa na sherehe fupi kama protokali na sheria za mapokezi ambapo kutakuwapo na midundo ya ngoma za utamaduni na michezo. Karibia waamini 2000 watamsubiri Baba Mtakatifu katika uwanja wa ndege, baada ya masaa 13 ya safari! Tarehe 24 Januari itakuwa ni sherehe za makaribisho katika jumba la rais ili kukutana na rais na baadaye katika ofisi ya Cansela, ambapo watafanya mkutano na viongozi na Baba Mtakatifu atahtubia.

Karibu na Kanisa la Mtakatifu Francis wa Assisi Mkutano na maaskofu wa Celam na hotuba. Mchana atakuwa katika forodha na maadhimisho mapokezi ya Siku ya vijana na ambapo watawakilishwa watakatifu wasimamizi wa Siku ya Vijana, kati yao Mtakatifu Romero, Yohane Paulo II na Don Bosco ameeleza Bwana Gisotti. Baada ya siku ya sakramenti ya upatanisho tarehe 25 Januari, itafanyika hata Njia ya Msalaba na vijana katika Uwanja wa Mtakatifu Maria Antigua (forodhani).

Baadaye Baba Mtakatifu atapata chakula cha mchana na baadhi ya vijana kutoka mataifa mbalimbali, kabla ya kuanza mkesha katika uwanja wa Mtakatifu Yohane Paulo II mahali ambapo wanatarajia kutoa ushuhuda za aina tatu: mama mmoja wa familia atazungumzia juu ya thamani ya kulinda maisha, kijana aliyenusurika kutoka na madawa ya kulevya atazungumzia juuu ya uhuruma Mungu ilivyo mkomboa maisha yake, na mwisho atakuwa ni kijana kutoka nchini Palestina ambaye atazungumzia juu ya matatizo kwa kijana kuishi katika kanda hiyo.

Tarehe 27 Januari Misa itafanyika katika eneo hilo ambapo mara baada ya misa watatangaza mahali itakapofanyika Siku ya Vijana duniani ijayo na baadaye kutembelea huko Hogar kwa chakula cha mchana na baada ya chakula kutakuwapo na  mkutano na watu wa kujitolea katika Uwanja wa Rommel Fernandez Juan Diaz. Hiyo itakuwa ni fursa ya hotuba ya mwisho ya Baba Mtakatifu mjini Panama kabla ya kuondoka kwenda uwanja wa ndege wa Tocumen tayari kurudi mjini Vatican.


Maoni


Ingia utoe maoni