Alhamisi. 21 Novemba. 2024
feature-top
Papa Francisko anaomboleza vifo vya wahamiaji 170 waliokufa maji kwenye Bahari ya Mediterrania.

Bahari ya Mediterrania imegeuka kuwa ni kaburi la maisha na matumaini ya watu wanaokimbia vita, ghasia, umaskini, dhuluma, nyanyaso pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi. Taarifa za hivi karibuni zinaonesha kwamba, kuna watu wengine 117 wamezama na kufa maji nje kidogo ya Pwani ya Libya, kati yao kuna watoto na wanawake.

Mara tu baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa masikitiko na majonzi makubwa, Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 20 Januari 2019, amewakumbuka na kuwaombea wakimbizi na wahamiaji 170 waliokufa maji kwenye Bahari ya Mediterrania wakiwa njiani kutafuta: hifadhi, usalama na maisha bora zaidi. Pengine anasema Baba Mtakatifu, hii ni kazi ya wafanyabiashara ya binadamu na viungo vyake. Ametumia fursa hii kwa ajili ya kuwaombea viongozi wenye dhamana na wajibu kwa wakimbizi na wahamiaji kutekeleza vyema dhamana hii ili kuokoa maisha ya watu.

Bahari ya Mediterrania imegeuka kuwa ni kaburi la maisha na matumaini ya watu wanaokimbia vita, ghasia, umaskini, dhuluma, nyanyaso pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi. Taarifa za hivi karibuni zinaonesha kwamba, kuna watu wengine 117 wamezama na kufa maji nje kidogo ya Pwani ya Libya, kati yao kuna watoto na wanawake. Watu wengine 53 wamekufa maji kwenye Bahari ya Alboran, iliyoko kati ya Morocco na Hispania. Wengi wao ni wahamiaji na wakimbizi kutoka Barani Afrika.


Maoni


Ingia utoe maoni