Jumapili. 24 Novemba. 2024
feature-top
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kwamba, operesheni okoa ya DustD2 Hoteli imekamilika.

Watu zaidi ya 14 wameuwawa kutokana na shambulizi la kigaidi lililotokea katika hoteli ya DusitD2 eneo la 14 Riverside Drive, Jijini Nairobi siku ya Jumanne, tarehe 15 Januari 2019. Kuna idadi kubwa ya wananchi wa Kenya wamejeruhiwa kutokana na shambulizi hili, lakini watu zaidi 700 waliweza kuokolewa.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Siku ya Jumatano, tarehe 16 Januari 2019 amesema, watu zaidi ya 14 wameuwawa kutokana na shambulizi la kigaidi lililotokea katika hoteli ya DusitD2 eneo la 14 Riverside Drive, Jijini Nairobi siku ya Jumanne, tarehe 15 Januari 2019. Kuna idadi kubwa ya wananchi wa Kenya wamejeruhiwa kutokana na shambulizi hili, lakini watu zaidi 700 waliweza kuokolewa.

Magaidi wote waliohusika kwenye shambulizi hili wameuwawa na kwamba, hali kwa sasa ni shwari na salama, wananchi wanaweza kurejea kwenye maeneo yao kazi na kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Rais Kenyatta ametangaza kwamba, operesheni okoa imekamilika na ametumia fursa hii kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama nchini Kenya kwa kazi kubwa vilivyofanya kuokoa maisha ya watu. Vitendo vya kigaidi vina hatarisha amani, usalama na mafungamano ya wananchi! DustD2 Hoteli ni Jengo maarufu sana Jijini Nairobi ambamo watu wengi wanaweza kujipatia huduma ya bar, migahawa, ofisi na huduma za kibenki. Bwana Fred Matiang’i, Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya, anasema, hali ya usalama na utulivu imerejea tena, baada ya vikosi vya ulinzi na usalama kupambana kufa na kupona na magaidi wanaotishia amani na usalama wa raia na mali zao!

Maoni


Ingia utoe maoni