Tarehe 14 Januari 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Maaskofu katoliki kutoka nchini Chile na kuwahimiza juu ya njia ya kufuata katika mchakato wa mazungumoza na ujenzi wa Kanisa na jamii. Askofu Ramos Pérez katika mahojiano anaonesha furaha yake katika mkutano huo
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na maaskofu katoliki kutoka Chile wakiwa mjini Vatican ambapo wamezungumza na kujadiliana karibu muda wa saa moja na kupata chakula cha pamoja katika Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican. Mkutano wao ulikuwa ni muda mwafaka wa kubadilishana mawazo na kushirikishana katika mchakato wa ujenzi wa Kanisa lao. Ni siku ya Jumatatu tarehe 14 Januari 2019, saa tano kamili, Baba Mtakatifu aliweza kuzungumza na maaskofu watano kutoka Kamati ya kudumu ya Maaskofu wa Chile kama ifuatavyo:Askofu Santiago Jaime Silva Retalames, Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini huko, Askofu Mkuu René Osvaldo Rebolledo Salinas, Askofu wa Jimbo Kuu la Serena, na makamu Rais wa Baraza hilo Kardinali Ricardo Ezzati Andrello, Askofu Mkuu wa Santiago ya Chile, Askofu Juan Ignacio González Errázuriz wa Jimbo la di Mtakatifu Bernardo na Askofu Luis Fernando Ramos Pérez, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Chile wa Tetci, na Msimamimiz wa Kitume wa Rancagua, na ambaye ametoa taarifa katika mahojiano na Vatican News.
Mkutano wa faragha
Mkutano wao wa faragha na milango ikiwa imefungwa ambapo Baba Mtakatifu ameweza kuendeleza mazunngumzo yao katika kukabiliana na mantiki tofauti na wajumbe maaskofu kutoka nchini Chile na mazungumzo yao yaliyosaidia kuwa na tathimini juu ya safari ya Kanisa na nchi ya Amerika ya Kisini kutokana na miezi minane ya mwisho yaani tangu walipokutana naye mwezi Mei ambapo Baba Mtakatifu likuwa ameitisha mkutano ili kuzungumza juu ya manyanyaso ya kijinsia.
Katika mahojiano na Askofu Luis Fernando Ramos Pérez) anamethibitisha kuwa ukuu wa mazungumzo kindugu kati yao na Baba Mtakatifu yamekuwa muhimu sana. Na hii hasa ni mara baada ya mkutano wao uliofanyika mwezi Novemba 2019 wa maaskofu wote wa Baraza la Maaskofu wa Chile waliamu kuwa, ilikuwa vizuri wafike mjini Vatican, Kamati ya kuduma ya maaskofu ambayo imeundwa na watu watano, ili kuweza kuzungumza na Baba Mtakatifu na kumjulisha kwa jinsi gani mambo ya Kanisa la Chile yanakwenda tangu mwezi Januari 2018 wakati Baba Mtakatifu alipofanya ziara ya Kitume katika nchi hiyo hadi sasa.
Ni mazungumzo muhimu na kupata ushauri wa mang’amuzi
Kwa hakika mkutano ulikuwa ni muhimu sana na mazungumzo yenye mwafaka na Baba Mtakatifu kwa maana ya kuweza kumsimulia kidogo mang’amuzi ambayo hadi sasa Kanisa la Chile imechukua na inaendelea kwa namna gani na inatarajia nini kwa kipindi cha mwaka 2019 na 2020 wakati watakapofanya Mkutano wa Kanisa nchini Chile. Baba Mtakatifu Francisko amewasikiliza historia yao na kuwapa ushauri mwingi unaotokana na hekima na utambuzi wa mambo mengi. Kwa maana hiyo amethibitisha kwamba wanaweza kusema ni ushauri mwingi waliopewa hasa wa mambo madogo madogo, lakini ambayo yanaangaza zaidi katika mazungumzo na Baba Mtakatifu.
Mkutano wa Marais wa Mabaraza ya Maaskofu duniani Februari 2019
Kuhusiana na mkutano maalum wa Rais wa Mabaraza ya Maaskofu duniani kwa ajili ya ulinzi wa watoto, unaotarajiwa kufanyika mwezi Februari 2019, Askofu anathibitisha kwamba huo ni mwaliko wa Baba Mtakatifu na ni kwa ajili ya Marais wa Baraza la maaskofu wote duniani, lakini Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Chile alimteua wa kumwakilisha na ambaye tayari ni yeye yuko katika shughuli hiyo kama Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu,na kwa maana hiyo amethibitisha jyy ya kujuandaa vema katika kuweza kutoa majibu kwa uangalifu.
Lakini hata hivyo amebainisha kuwa wanapaswa kufanya mchakato wa mapokezi na mazungumzo kwa waathirika wa manyanyaso ya kijinsia ambapo kwa sasa wako wanafanya kazi juu ya suala hilo… Askofu anahitimisha kwa kusema kuwa, anaamini kwamba utakuwa ni mkutano muhimu kwa ajili ya Kanisa duniani na kusaidia kila Kanisa mahalia kuwa na utambuzi wa jinsi gani ya kujikita katika uwazi na akili mbele ya hali halisi kama hizo ambazo ni uhalifu mkubwa.
Maoni
Ingia utoe maoni