Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, anawaombea wale wote walioguswa na kutikiswa na shambulizi hili na anapenda kuwahakikishia uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake. Baba Mtakatifu anaiombea familia ya Mungu nchini Kenya nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu!
Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya shambulizi la kigaidi lililotokea katika hoteli ya DusitD2 eneo la 14 Riverside Drive, Jijini Nairobi siku ya Jumanne, tarehe 15 Januari 2019 na kusababisha watu zaidi ya 15 kupoteza maisha na watu zaidi ya 36 kujeruhiwa vibaya.
Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, anawaombea wale wote walioguswa na kutikiswa na shambulizi hili na anapenda kuwahakikishia uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake. Baba Mtakatifu anaiombea familia ya Mungu nchini Kenya nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu!
Maoni
Ingia utoe maoni