Mara baada ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Januari 2019, amewakumbusha waamini na mahujaji juu ya wiki ya kuombea umoja wa Wakristo itakayoanza tarehe 18-25 Januari 2019. Amewahimiza kuiishi wiki hiyo kwa maombi ya kina
Mara baada ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 16 Januari 2019, amewakumbusha waamini na mahujaji kuwa, Ijumaa tarehe 18 Januari inaanza Wiki ya kuombea Umoja wa Wakristo itakayofunguliwa na maadhimisho ya Masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo, Roma.
Mada inayoongoza maombi hayo ni “tafuteni haki ya kweli”. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kwamba, hata mwaka tunaalikwa kusali ili wakristo wote warudie kuwa familia moja ya dhati kwa utashi wa Mungu anavyopenda kuwa wote wawe wamoja, (Yh 17, 21). Aidha ameongeza kusema kuwa, Uekumene siyo jambo la uchaguzi. Lengo litakuwa ni lile la kukuza muungano na maelewano ya ushuhuda wa kuthibitisha haki ya kweli na katika kutoa huduma kwa kuwasadia walio wadhaifu zaidi kwa njia ya kutoa jibu la dhati linalostahili.
Maoni
Ingia utoe maoni