Jumatano. 11 Septemba. 2024
feature-top
Mkutano wa kimataifa hulo Berlin Ujerumani katika kutafuta suluhisho la kipeo cha mapigano nchini Libya tarehe 19 Januari 2020

Baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa Francisko amewatakia matashi mema na ufanisi wa Mkutano wa Kimataifa huko Berlin, Ujerumani,kuhusu kipeo cha Libya.Papa anawashauri wawe na safari njema ambayo iwapelekee kupata mchakato mwema wa suluhisho.Kati ya mambo aliyomo kwenye rasimu ya hati ya mwisho itakayosahiniwa na wakuu hao ni vikwazo juu ya silaha na kuanza kwa mchakato wa serikali ya umoja nchini Libya.

Mara baada ya tafakari ya neno la Mungu katika Jumapili ya Pili ya Mwaka A, tarehe 19 Januari 2020 kwa waamini na mahujaji wote waliokusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro, Vatican, Papa Francisko amekumbusha kuwa: “ jijini Berlin wanafanya mjadala kwa mara nyingine tena kuhusiana na kipeo cha Libya”. Kwa maana hiyo ni matumani hai kwamba mkutano huo muhimu, unaweza kuanzisha mchakato mwema katika kuelekea kusitisha vurugu za mapigano nchini Libya na kupata suluhisho la mchakato wa amani ambayo inatamaniwa kuwa na msimamo wa nchi hiyo.

Salam kwa mahujaji wote kutoka mataifa mbalimbali

Salam kwa mahujaji wote wa Roma na kwa namna ya pekee wajumbe wa  chama cha  Sevilla, kutoka Uhisipania; waamini kutoka Bielsko-Biała na  Poznań, Poland, wanafunzi wa Chuo cha “Loras, cha Dubuque, Marekani, na wale wa Vila Pouca de Aguiar, Ubelgiji; makundi mengi ya kiparokia na majimbo kutoka nchini Italia.

Mwaka 2020 kwa ajili ya wauguzi na wakunga

Papa Francisko aidha ameonesha kupendezwa na chaguo la mwaka 2020 kutolewa kwa ngazi ya kimataia kama ‘Mwaka wa Wauguzi na Wakunga’. Papa amesema: “ “Ninafurahi kukumbuka kuwa 2020 kwa ngazi ya kimataifa umechaguliwa kama mwaka wa wauguzi na wakunga. Wauguzi na wakunga ni wahudumu wa afya wengi ambao  labda wanatimiza kazi muhimu sana kati ya taaluma zote”. Kwa maana hiyo Papa ameongeza kusema: “ Tuwaombeee wote ambao wako karibu na wagonja zaidi ili waweza kutenda kazi yao vema yenye thamani kubwa”. Na kwa wote Papa  anawatakia kila heri na baraka ya Jumpaili, lakini akiwatakia mlo na mchana mwema na wasisahau kusali kwa ajili yake.

Kuhusiana na Mkutano wa Berlin

Wadau muhimu wanakutana  Jumapili  19 Januari 2020 mjini Berlin Ujerumani ili kujadili makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Libya yanayoyumbisha nchi hiyo. Wakati huo huo washiriki kwenye mkutano huo wanataka kutafuta njia ya kukabiliana na nchi za kigeni zinazoingilia kati masuala ya nchi hiyo inayokumbwa na machafuko tangu kuzuka ghasia za kuipinga serikali za mwaka 2011 zilizoungwa mkono na nchi wanachama wa jumuiya ya kijeshi NATO. Ujerumani na Falme za Kiarabu (UAE) zimetoa wito wa pamoja kwa pande zote katika mzozo wa Libya kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa ya kusitisha mapigano ya muda mrefu na kwa vikosi vya kigeni kuondoka nchini humo.

Suluhisho linaweza kufikiwa kwa njia ya mazungumzo

Msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Seibert kabla ya Mkutano huo kuhusu amani ya Libya kwa viongozi wa kimataifa amesema wito huo ulitolewa baada ya kufanyika mkutano kati ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na mwanamfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed al Nahyan. Viongozi hao wawili wamesisitiza kwamba mzozo wa Libya hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi, bali kwa kudumisha amani na utulivu ambavyo vitafikiwa kwa njia ya mazungumzo. Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan amesema Falme za Kiarabu zingefanya kila jitihada kusaidia utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa Berlin kuhusu Libya. UAE ni mmoja wa washirika muhimu zaidi wanaomuunga mkono kiongozi wa waasi jenerali Khalifa Haftar ambaye vikosi vyake vinadhibiti sehemu kubwa ya Libya na wanaipinga serikali ya Waziri Mkuu Fayez al-Serraj iliyopo katika mji mkuu wa Libya, Tripoli inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano huo wapo wadau kutoka sehemu mbali mbali za dunia

Mkutano huo wa kilele wa Berlin umeandaliwa kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, anayeongoza mashauriano ya kutafuta suluhisho la amani juu ya mzozo wa Libya pamoja na mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia masuala ya Libya Bwana  Ghassan Salame. Wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 10 wanashiriki katika mazungumzo hayo ya amani ya Libya yaliyoandaliwa na kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Kwa maana wawakilishi ni kutoka, Algeria, China, Misri, Fslme za nchi za Uarabuni Ufaransa, Italia, Uingereza, Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo DRC Urusi, Marekani na Uturuki. Aidha wamewahusisha mashirika ya Kimataifa kama vile Ligi ya Urabuni, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya. Tunisia haitashiriki, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo na kwamba hatua hiyo ni kutokana na kupokea mwaliko dakika za mwisho kabla ya mkutano huo kuanza. Hata hivyo ikumbukwe kwamba Libya yenye utajiri mkubwa wa mafuta imekuwa kwenye machafuko tangu kuondolewa na kuuawa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mnamo mwaka 2011. Pande mbili zinazopingana na makundi mengine kadhaa ya wanamgambo wote wanapigania kuitawala Libya. Serikali ya umoja wa kitaifa inayotambulika kimataifa iko mjini Tripoli wakati Jenerali muasi Khalifa Haftar anaungwa mkono utawala wa eneo la mashariki mwa Libya.

Mada sita msingi

Katika masaa haya kwenye vyombo vya habari vya kimataifa vinazungukia juu ya rasimu ya tamko la mwisho na ambalo saini ya washiriki inangojewa ikiwa na hoja kuu sita: kudumisha suala la kusitisha mapigano, kuheshimu na vikwazo vya utolewaji wa silaha na kuanza tena mchakato wa kisiasa ili ufikie kupata serikali ya umoja, mageuzi katika nyanja ya usalama, mageuzi ya kiuchumi, heshima za haki za binadamu. Hata hivyo rasimu ya hati hiyo inaweza bado kuwa na mabadiliko wakati shughuli ya mkutano huo wa wanadiplomasia.


Maoni


Ingia utoe maoni