Jumatano. 04 Desemba. 2024
feature-top
Papa Francisko amekumbuka akiwa ametulia katika sala wakati wa kutembelea kambi ya mauaji ya kimbari huko Auschwitz,Poland tarehe 29.07.2016

Papa Francisko amekutana mjini Vatican na uwakilishi wa Kituo cha Simon Wiesenthal na kuweka bayana juu ya kuendelea kulaani kila aina na vitendo vya ubaguzi.Kituo hiki kwa miaka mingi kinajikita na jitihadza za kupambana na kila aina ya ubaguzi na chuki dhidi ya walio wachache.Anawaalika kuwa wapanzi wa amani na kukuza pamoja ule udugu hasa mbele ya ukatili dhidi ya wayahudi.

Papa Francisko tarehe 20 Januari 2020 amekutana na uwakilishi kutoka kituo cha Simon Wiesenthal. Ni kituo ambacho kinashughulika duniani kote katika mapambano dhidi ya kila aina ya ubaguzi, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya watu walio wachache. Papa anasema, ni kwa miaka kumi sasa kituo hiki kinashirikiana  na Vatican. Na mambo yanayowaunganisha ni ile shauku za kuona dunia inakuwa mahali bora, heshima ya hadhi ya binadamua na hadhi ya kuheshimu kila mmoja kadili alivyo kutegemea na asili yake, dini yake,na namna yake ya kuishi kijamii. Na ni muhimi sana kufundisha kuvumilia na kuelewana kwa pamoja, uhuru wa kidini na kukuza amani kijamii.

Pongezi kwa mchango wao wa kutunza kumbu kumbu

Papa Francisko aidha anawasifu kwa mchango wao kwa namna ya pekee wa kutunza ari ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari. Na pia kukumbusha juu ya tukio la  tarehe 27 Januari  ambapo watakuwa wanaadhimisha miaka 75 tangu kupata uhuru kutoka katika kambi ya kibaguzi ya mauaji huko Auschwitz-Birkenau. Kwa kukumbuka ziara yake nchini Poland katika kambi hiyo Papa amebainisha ni kwa jinsi gani alikaa na kusali kwa kina. Leo hii katika kusongwa na mambo mengi  amongeza kusema, tunashindwa kukaa na kujitazama kwa ndani, kujifafanua kwa ukimya ili kusikiliza kilio cha binadamu anayeteseka”. Maneno  ya kisiasa yamekuwa  mengi na wakati mwingine yasiyo kuwa na faida, na wakati huo hata kupoteza muda kwa kupiga kelele bila kupima yale ambayo yanazungmzwa. Ukimya badala yake  Papa amesema - unasaidia kuhifadhi kumbu kumbu.

Tunapoteza kumbu kumby na kuharibu wakati endelevu

Tunapoteza kumbu kumbu na kuharibu wakati endelevu. Kufanya kumbu kumbu ya mwaka kuhusiana naukatili usiosahaulika  na ambao binadamu aliugundua miaka 75 iliyopita ni mwito kwa hakika wa kusimama na kukaa kwa  kimya na kufanya  kumbukumbu. Hii inasaidia na siyo kuwa na sintofahamu, amehimiza Papa Francisko. Wasi wasi unazidi kuongezeka katika sehemu mbalimbali za dunia za  sintofahamu ya unafiki na ile tabia ya kujali kile tu kinachokuwa bora binafsi. “Maisha yanakuwa mazuri pale mambi yanapokwenda vizuri, lakini yakienda mrama basi ndiyo kuzuka kwa hasira na ukatili. Na hivyo ndiyo kuandaa ardhi yenye rutuba kwa namna ya ubaguzi ambao tunaouona umetuzunguka. Katika ardhi hizi chuki zinakua kwa haraka”.

Sitoacha kulaani kila aina ya mtindo wa ubaguzi

Papa Francisko akiendeea amesema, hatacha kulaani kwa nguvu kila mtindo wa ubaguzi. Na ili kukabiliana na tatizo la mzizi  amesema tunapaswa lakini kuwajibika kwa dhati hata katika ardhi ambazo zinazidi kukua kwa chuki ili kupanda mbegu ya amani. Kwa hakika kwa njia ya ufungamanisho, utafiti na uwelewa wa mwingine ambaye analinda kwa kiasi kikubwa sisi wenyewe. Kwa njia hiyo ni dharura ya kufungamanisha na  yule ambaye amebaguliwa, kumfungulia mikono yule aliye mbali,  kumsaidia aliyewekwa pembeni kwa sababau hana zana za fedha, kumsaidia aliye mwathirika wa uvumilivu na ubaguzi.

Wakristo na Wayahudi tuna utajiri wa urithi mmoja wa kitasaufi

Hati ya Nostra aetate (4) inasisistiza kuwa Wayahudi na Wakristo tuna utajiri wa urithi mmoja wa kitasaufi ambao tunapaswa kuugundua daima na kuweza kuuwekwa katika huduma ya wote, amesemaPapa. Kufuatia na hiyo ndipo mwaliko wake kwa namna ya pekee kuwa mstari wa mbele katika huduma hiyo. Anawahimiza wasiwe mbali na kubagua, badala yake wasimame kidete na kuunganisha , wasifurahia suhuhisho la nguvu, badala yake waanzishe michakato ya kukaribiana. Ikiwa hatufanyi sisi,amesema,  ambao tunaamini Yule aliye juu , ambaye alitukumbuka na kujali kwa moyo wake udhaifu wetu, je ni nani atafanya hivyo?  Ni swali la Papa . Lakini pia kwa kukumbuka  maneno ya  Agano la Kale katika Kitabu cha Kutoka  yasemayo : Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia. (Kut 2,24-25). Papa amehitimisha kwa kuwashukuru kwa juhudi zao na kuwatia moyo ili wawendelee katika ushirikiano wa kulinda walio dhaifu zaidi. Na Aliye juu atusaidia kuheshimiana na kupendana zaidi na zaidi na kuifanya ardhi tunamoishi iwe bora, huku tukipambania amani. Shalom!


Maoni


Ingia utoe maoni