Jumamosi. 23 Novemba. 2024
feature-top
Wahamiaji wanaofika mpakani McAllen, Texas mara nyingi ni familia na watoto wao, ni watu wenye historia yao wenye sura, ni binadamu na siyo namba au wahalifu

Sr. Norma Pimentel ambaye anajulikana hata kwa upande wa Baba Mtakatifu kutokana na shughuli yake ni Mkurugenzi wa Caritas ya Rio Grande na Mhusika wa Kituo cha mapokezi ya wahamiaji na wakimbizi, amemwandikia Barua Rais wa Marekani Bwana Donald Trump siku aliyotembelea McAllen Texas mpakani mwa Marekani na Mexico

Mkurugenzi wa Caritas wa Rio Grande na mhusika wa kituo cha kibinadamu Sista Norma Pimentel amemwandikia Rais Donald Trump siku ambayo amefanya ziara yake huko McAllen, Texas, kituo ambacho ni mpaka na kwa mujibu wa rais ndipo wanataka kujenga ukuta wa kutengenisha. Sr Norma ambaye anajulikana hata kwa upande wa Baba Mtakatifu kutokana na kwamba siku moja katika Katekesi yake alimwita kati ya watu wengi ili kumshukuru, kwa maana katika kituo chake amewapokea zaidi ya wahamiaji 100elfu kwa miaka minne ya mwisho, kwa maana ya kusema kuwa ni wahamiaji 300 kila siku. Barua inaanza kusema kuwa, mpendwa Rais tunakukaribisha katika jumuiya yetu ya Kusini mwa Texas, katika Rio Kubwa ambayo inaunganisha Marekani na Mexico. Ninakukaribisha kututembelee.

Kituo cha mapokezi kilifunguliwa kunako 2014
Katika barua yake Sr. anasema kuwa milango ya kituo cha mapokezi kilifunguliwa kunako 2014 wakati makumi elfu ya watu wakitokea Guatemala, Honduras na El Salvador, wakikatisha mpaka na kusababisha dharura kubwa katika eneo hilo la Rio Kubwa. Hawa walikuwa ni familia za wahamiaji, wenye njaa, wanaoogopa ambapo baadaye wanakwenda kwenye vituo vy mabasi wakiwa na nguo moja tu waliyovaa na hawakuwa na chakula na wala cha kunywa. Sr Norma na jumuiya za kikirsto, lakini pia hata masharika mbalimbali walianza kwa haraka kuhakikisha angalau watu hawa wanapata mlo na huduma ya kwanza, ambapo baadaye kimekuwa kituo ambacho yeye mwenyewe anaongoza. Wakati familia zilikuwa zikipita kwa ujumla walikuwa wanakamatwa na mamlaka mpakani na baada ya siku kadhaa walikuwa wanaawachia wakiwa na hati fulani iliyokuwa imeidhinishwa na mahakama ya kuchunguza maombi yao hifadhi.Mara baaada ya kuachwa mpakani wahamiaji wanapokelewa katika kituo hicho. Kwa kawaida walipokuwa wamefika katika milango sehemu kubwa ya watu wazima walikuwa wamefungwa mkanda wa wa Kieletroniki mguuni unaotolewa na polisi mpakani wakati huo wakibeba chaji kubwa ya kutunza kifaa hicho cha kieletriniki kufanya kazi yake.

Barua siyo ya hasira bali inaelezea hali halisi
Katika barua yake haioneshi hali ya kuhukumu uhalifu, wala wageni bali inaelezea hali halisi ya wahamiaji hao. Kwa maana hiyi katika barua hiyo inaelezea familia zinazofika katika kituo kwa mara ya kwanza wanafikia wakiwa na hofu kubwa wakiwa na vitu vitogo sana vilivyofungwa katika mfuko wa plastiki tu. Watu wanaofika ni walio wachache wanazungumza kingereza, wakati huo wengi wao wanasafiri na watoto wadogo. Aidha amemwonesha hali halisi ya kituo hicho katikati ya Uwanja wa El Paso mahalia ambapo siku zilizopita yaani mwanzo wa mwaka, maelfu ya wahamiaji wameachiwa na mamlaka ambapo kama Rais umeona na kuzungumza. Kwa maana hiyo Sr anasisitiza jinsi gani mapema asubuhi wanaonekana familia nyingi zinazofika wakati wa usiku wanaamka na kutengeneza vema nafasi walizolala. Wanafamilia wanasaidia kuandaa chai ya asubuhi wengine wanajiandaa kuanza safari kwa Bus kuelekea nchi nyingine. Watu wa kijitolea wakiandaa mifuko ya vitu vya kuwasaidia kama chakula kwa mfano wakiandaa mikate na mboga za majani, wengine mchuzi na kwa ajili ya chakula, lakini wengine pia wakindaa vema nguo zilizoletwa kwa ajili ya wahamiaji. Wengine wanasaidia kutafuta mawasiliano ya familia ndugu ambao wanaishi tayari mwaka na kuwaandalia tiketi,au vibao vidogo vyenye kuandikwa: “saidie, mimi sizungumzi kingereza, “Je ni bus gani nichukue, asante kwa msaada wako”.

Askofu Mkuu Joseph W.Tobin wa Jimbo Kuu Katoliki la Newark Marekani
Nimesikiliza kwa kina kukatishwa tamaa na maneno yasiyo ya kibindamu yaliyotumia kuelezea ndugu zetu na dada wahamiaji. Wanaume, wanawake na watoto siyo namba na wala takwimu za wahalifu, bali ni watu wenye kuwa na mwili na mfupa, Ni watu wenye kuwa na uzoefu binafsi na historia zao. Sehemu kubwa ya watu hawa wanakimbia majanga ya kibinadamu na ghasia mbaya zinazohatarisha maisha yao. Maandishi na sentensi katika mabango za kuogopesha zilikuwa zinataka kuonesha kwa namna ya pekee kama vile nchi yetukubwa inasaliti mizizi yaotu kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi.

Huo ni uthibitisho wa maneno ya Askofu Mkuu Joseph W.Tobin wa Jimbo Kuu Katoliki la Newark Marekani akitafakari juu ya maneno ya Rais wa Marekani Bwana Donald Trump kwenye ujumbe wake wakati akihutubia taifa Jumanne tarehe 8 Januari 2019 kuhusiana na suala la wahamiaji katika mpaka wa Marekani na Mexico, na ambapo anayo nia ya kujenga ukuta. Ujumbe wa Rais wa Marekani aliposhambulia wahamiaji wa Amerika ya Kati wanaotafuta nama ya kuweza kuingia ndani ya nchini na kuomba hifadhi, au watu wanakimbia hali halisi mbaya ya umasikini siyo suala la namna ya kuwekwa katika majadiliano ya kisiasa, ni wageni na jirani zetu ambao Maandiko matakatifu yanahamasisha mara kwa mara kuwa na mapokezi na kwa maana hiyo Askouf Mkuu anaomba kama mchungaji wa watu wa Mungu Kaskazini ya Jimbo la New Jersey na ndugu viongozi wote wa kisheria kuungana kwa ajili ya wema wa pamoja. Waungane kwa pamoja bila kuchoka licha ya tofauti zilizopo kwa ajili ya wema wa wote kwa maana maisha yao yanategemeana kwa dhati na hili.

Ziara ya Trump huko McAllen huko Texas
Ziara hiyo inakuja wakati huu sehemu ya shughuli za serikali zikiwa zimefungwa kufuatia kutoafikiana juu ya fedha za ujenzi wa ukuta huo. Alhamisi 10 Januari 2019, Trump alikutana na maafisa wa doria ya mpakani kwenye jiji la McAllen. Wakati huo alisisitiza kuwa ujenzi wa ukuta huo ni muhimu, iwe ni ukuta wa chuma ama zege. Trump pia alikikosoa chama cha Demokrat na vyombo vya habari kwa kumtuhumu kuwa amezalisha mgogoro huo wa mpaka. Hata hivyo awali rais huyo alitaka kuwepo na maafikiano kutoka Demokrat kwa kutishia kutumia mamlaka yake kutangaza hali ya dharura ya taifa na kujenga ukuta bila ya kupata idhini ya Bunge la Congress. Lakini kwa pande mbili hizo zimeendelea kutofautiana kwa kiasi kikubwa.

Ujenzi wa ukuta ni sehemu ya mpango wake wa kampeni ya uchaguzi
Rais Trump wa Marekani amefanya ziara katika mpaka na Mexico ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kujenga ukuta,siku moja baada ya kutoka katika mkutano wa majadiliano wakati wapinzani wa ujenzi huo kutoka chama cha Democratic. Na wakati huo ni mamia kwa maelfu ya wafanyakazi wa serikali wanakabiliwa sasa na kukosa mishahara yao. Ijumaa 11 Janauri 2019 akiwa mjini McAllen , Texas , Trump ametembelea kituo cha mpakani cha doria kwa ajili ya mazungumzo kuhusiana na uhamiaji na usalama wa mpakani, na kupata maelezo kuhusu usalama wa mpaka. Bwana Trump hataki kisikiliza ushauri wa yoyote kutokana na kwamba ujenzi wa ukutua ni ahadi yake kuu tangu alipokuwa akifanya kampeni ya urais.

Maoni


Ingia utoe maoni