Tarehe 2 Machi 2019 katika mji Mkuu wa Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imezinduliwa Hospitali ya Watoto na Kardinali Konrad Krajewski, mtunza sadaka mkuu wa Papa kwa niaba ya mshikamano na Baba Mtakatifu Francisko ambapo kama alivyosema katika ujumbe wake kwa njia ya video kuwa Hospitali hiyo ni matunda ya Mwaka wa huruma ya Mungu! Aidha katika ujumbe wake kwa njia ya Video, ameonesha ni kwa jinsi gani aliguswa na mateso na taabu za watoto wadogo wakati akiwa akiwa nchini Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati kunako mwaka 2015 na ambapo alifungua mlango wa Kwanza wa Huruma katika Kanisa kuu la Bangui badala ya Mlango wa Mtakatifu Petro uliofungulia baadaya ya kutoka Ziara hiyo.
Katika sherehe za uzinduzi huo, kutoka Vatican wamemwakilisha Baba Mtakatifu, Kardinali Konrad Krajewski, mtunza sadaka mkuu wa Papa, akiambatana na Dr. Mariella Enoc, Rais wa Hospitali ya Bambino Gesù inayomilikiwa na kuendeshwa na Vatican, Kamanda Domenico Giani, Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama mjini Vatican waliosaidia sana hupatikanaji wa fedha za ujenzi wa Hospitali hii.
Hospitali ni ishala ya matumaini kwa watoto wa Bangui: Katika mahojiano na Bi Enoc Rais wa Hospitali ya watoto Bambino Gesu akiwa huko Bangui anafafanua juu ya kutimiza mpango huo na ambao ulitangazwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa ziara yake nchini Jamhuri ya Kati na ikiwa ni fursa ya kuzindua Mwaka wa Jubilei ya Huruma. Bi Enoc anathibitisha kuwa ni tunda la mchakato mgumu wa miaka miwili na nusu na ambao ni furaha kubwa kuona jengo hili limekwisha na kuwa na wahudumu mahalia, wafanya kazi, wataalam na wote ambao wamewezesha kweli kufikia kukamilika kwa jengo hilo maalum katika ardhi ya Afrika.
Ni matashi ya Bi Enoc ya kwamba wanaweza kuendelea kufuatilia na kutoa msaada katika kituo cha afya kwa mafunzo makubwa na kinaweza kuwa kituo cha kipekee cha tiba katika moyo wa Afrika, mahali ambamo kunaonekana uharibifu na umasikini. Hiki ni kituo cha matumaini kwa ajili ya watoto; na kila kitu kimefanyika kwa vipimo vya watoto, ukubwa na uzuri wake ili kuweza kuunda furaja kwa wadogo kwa sababu hata kama wako hospitali, hata hivyo ni kidogo kama inavyo jionesha hata Roma katika Hospitali ya watoto Bambino Gesu, upendo na uzuri unawasaidia kuwa na furaha kwa wakati watoto hao.
Katika jengo hili jipya ambalo limekarabatiwa na kupanulia, Bi Enoc kwa ujumla anathibitisha kuwa ni Hospitali ya watoto ya kutibu magonjwa yote mahalia. Na shughuli yake ni kujikati katika dawa, upasuaji na magonjwa yote ambayo katika nchi hizi kwa namna ya pekee yameenea, na ambapo watajitahidi kufanya vizuri zaidi na kwa maana hiyo ni lazima kutambua kuwa ni Hospitali ambayo kwanza lazima iangaikie magojwa yote ya watoto. Vilevile amaeelzea juu ya shughuli kwamba Hospitali hii ina kitengo cha watoto wagonjwa wa utapiamlo, licha ya kupewa tiba na lishe bora, lakini pia wanawake wataanza kufundwa namna ya kuwahudumia watoto wao wanaokabiliwa na utapiamlo wa kutisha. Vatican pia imeanza kulipa mishahara kwa madaktari na wafanyakazi wa hospitali ya watoto wadogo sanjari na ukarabati mkubwa wa miundo mbinu ili kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa watoto wagonjwa. Na ndiyo kiini msingi cha Baba Mtakatifu Francisko kuwakabidhi majukumu hayo Bi Enoc na wadau wengine katika mahitaji ya watoto wanaoteseka anathibisha katika mahojiano Bi Enoc Rais wa Hospitali ya watoto Bambino Gesu’ akiwa ziarani Afrika ya Kati katika uzinduzi wa Kituo hiki cha Afya nchini Afrika ya Kati
Maoni
Ingia utoe maoni