Balozi wa Afrika ya Kusini kwa Vatican,Bwana George Johannes amevutiwa sana na Baba Mtakatifu Francisko juu ya kuwa na kufahamu wa matukio yanayotendeka Afrika. Amethibitisha hayo akihojiana na Vatican News mara baada ya Baba Mtakatifu Francisko kukutana na wanadiplomasia pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vatican tarehe 7 Januari 2019
Kilichonigusa sana kwa Baba Mtakatifu Francisko ni tendo la kuona kuwa ana ufahamu wa kila matukio yanayotendeka Afrika. Ndiyo mwanzo wa jibu la Balozi George Johannes wa Afrika ya Kusini mjini Vatican katika mahojiano na Vatican News Jumatatu, tarehe 7 Januari 2019 mara baada ya kukutana na Baba Mtakatifu Francisko na kuzungumza na wanadiplomasia pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vatican.
Uwepo wako unabeba ujumbe Fulani kwa Afrika
Balozi wa Afrika ya Kusini Bwana Johannes wakati wa mahijiano kwenye Stufdia za Vatican News, amethibitisha kuwa amezungumza na Baba Mtakatifu Francisko na kumwambia kwamba:“ tunakuitaji Afrika…Uwepo wako hunabeba ujumbe fulani kwa Afrika”. Kutokana na hilo Balzoni anasema kuwa ni matarajio yake kwamba ziara nyingine katika nchi za Afrika, zinaweza kuongeza juhudi za amani na kuhimiza ushirikiano wa mataifa ambo ni wenye tishio kutokana na aina mpya ya mipasuko.
Afrika inakabiliana na aina mpya za mipasuko
Aidha akiendelea na mahojiano na kujibu maswali, Balozi George amethibitisha kuwa Baba Mtakatifu wakati wa hotuba yake, amezitaja nchi kadhaa ambazo kuna matatizo makubwa (Tunakabiliwa) na aina mpya za migawanyiko, ambazo jumuiya na jamii za Afrika zimevujika. Kwa maana hiyo Balozi George anathibitisha kwamba, kuna haja ya kutengezwa na kuongeza kusema kwamba anayo matarajio ya kwamba uwepo wa Baba Mtakatifu katika nchi za Afrika unaweza kuchangia maana kubwa ya kuelekea katika mchakato wa uponyaji.
Wahamiaji wa Afrika wanakimbia kutokana na matatizo halisi na makubwa
Balozi Johannes amesema kuwa, Baba Mtakatifu anajua hali halisi na mbaya inayaosababisha wahamiaji kufika Ulaya na kuongeza kusema: “Tunapoangalia matukio ya wale wanaokuja kwenye boti, unaona Waafrika, wakati huo huo kutokana na ujio wa waafrika hao kuna majibu yanayotolewa dhidi yao kutoka Ulaya. Sitaki kuwa mwanasiasa kuhusu hilo (lakini) tulikubali sana wakati walipokuja wakuu wa kikoloni walifika nchi zetu na mara nyingi, hata waliwazuia watu kuwa na ardhi yao na utamaduni wao na kuweka njia yao ya maisha kwa watu ya Afrika...Watu wanapaswa kukumbushwa kuhusu wapi tumetoka... (hawa) watu wanakimbia kutokana na matatizo halisi na makubwa katika Afrika na haya ndiyo mambo ambayo Baba Mtakatifu anatukumbusha na nadhani mtu anaweza kuhisi katika njia aliyokuwa akizungumza, wakati alipozungumzia masuala ya Afrika, kwamba alijihisi mateso sana juu yao”, alisema Balozi Johannes.
Mkutano wa mwaka kwa wanadiplomasia na wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu, tarehe 7 Januari 2019 amekutana na kuzungumza na wanadiplomasia pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vatican ambayo imekuwa ni sehemu ya mapokeo na utaratibu wa kutakiana heri kwa mwaka mpya wa 2019. Katika Mkutano huo na ambao kwa kawaida hotuba yake ya mwanzo wa mwaka kwa wanadiplomasia utarajiwa sana na mataifa mengi kwa maana inaonesha tayari ratiba kamili ya mwaka kwa upande wa shughuli za mahusiano ya kidiplomasia na nci, kwa maana hiyo Baba Mtakatifu aligusia kuhusu, Mikataba mbali mbali ambayo Vatican imetiliana sahihi na Nchi pamoja na Mashirika ya Kimataifa kama vile UNESCO ambayo kwa mwaka 2019 inaadhimisha kumbu kumbu ya Miaka 70 tangu kuanzishwa kwake.
Hali kadhalika Baba Mtakatifu Francisko amejikita kuelezea juu ya hija za kitume alizotekeleza katika kipindi cha mwaka 2018 na zile anazotarajia kuzifanya kwa Mwaka 2019 kwa lengo la kutaka kuimarisha mahusiano mema ya kidiplomasia. Naye mwanadiplomasia Balozi Armindo Fernandes do Espírito Santo Vieira Balozi wa Angola mjini Vatican ndiye aliyetoa utangulizi kwa niaba yao kabla ya Baba Mtakatifu kuanza hotuba yake .
Maoni
Ingia utoe maoni