Maandamano makubwa ya vijana mjini Bruxelles yamefanyika mwishoni mwa wiki hii ambapo kulikuwapo na vijana wa kila rika,yaani kuanza watoto wa shule za msingi hadi vyuo vikuu na wazee waliofika kuunga mkono maandamano ya wajuu zao.
Maandamano hayo kuhusu mabadiliko ya tabianchi yamefanyika tarehe 21 Februari 2019 mjini Bruxelles, ambapo maelfu ya vijana kutoka Ulaya nzima kwa nia moja ya kuomba ngazi ya kisiasa kujikita kwa dhati katika mapambano ya kuzuia mabadiliko ya tabianchi. Lengo kuu la tukio hilo lilikuwa ni kuomba kwa kiasi kukubwa haki ya mabadiliko ya tabianchi kwa kiwango cha kuweka jitihada kwa upande wa serikali zote na hatimaye kuweza kusimamisha kiwango cha joto la mabadiliko ya tabianchi. Aliyeongoza maandamano hayo ni kijana mdogo kutoka Sweden Greta Thunberg, mwenye umri wa mika 16 na ambaye alianza na mgomo mdogo wa kusimama mbele ya bunge la Sweeden lakini akaweza kupata nafasi ya kusikilizwa sauti yake na wakuu wa dunia.
Maneno ya Greta anasema: “Tanajua kuwa wanasiasa hawataki kuzungumza nasi. Ni vema, lakini hata sisi hatutaki kuzungumza nao. Tunachoomba kwao, wazungumze na wanasayansi na wawasikilize, kwa sababua sisi tunarudia kile ambacho wamekuwa wakikazia kwa miaka”. Hata hivyo kijana mdogo Greta alikutana na Rais wa Tume ya Umoja wa nchi za Ulaya Bwana Jean-Claude Juncker na ambaye pia amethibitisha kwamba: “kijana huyu ana huzuni, kwa sababu hadi leo hii, Taasisi ya Umoja wa nchi za Ulaya hatujafanya kiasi kikubwa kinachotakiwa kulinda hali ya hewa”.
Hata hivyo taarifa iliyochapishwa kwenye Tovuti ya WMO mwaka huu imesema miaka ya 2015, 2016, 2017 na 2018 imekuwa ya joto zaidi na kwamba hii ni ishara dhahiri kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaendelea. Uchambuzi wa WMO unaonyesha kuwa kiwango vya wastani vya nyuzi joto kwa vipimo vya selsiasi kilikuwa ni 1,0 juu ya viwango vya kabla ya miaka ya kuanzishwa kwa viwanda 1850 hadi 1900.
Akizungumzia mwenendo wa hali ya hewa, Katibu Mkuu wa WMO, Petteri Taalas alisema mwenendo wa muda mrefu ni muhimu kuliko kuangalia mwaka mmoja mmoja na kwamba taswira inaonyesha kuwa viwango vya joto vinapanda kwami “miaka 20 iliyo na joto zaidi imekuwa miaka 22 iliyopita. Viwango vya joto katika kipindi cha miaka minne iliyopita vimekuwa vya aina yake nje na ndani ya bahari". Bwana Taalas amesema viwango vya joto ni kiungo tu kwenye taswira kwani athari kubwa na mbaya zitokanazo na hali ya hewa viliathiri nchi nyingi na mamilioni ya watu na kusababisha athari mbaya kwenye uchumi na mazingira mwaka 2018.
Kwa mujibu wa WMO, matukio mengi ya hali ya hewa yanaambatana na matokeo ya moja kwa moja ya mabadilko ya tabianchi na hivyo ni muhimu kukabiliana na hali halisi. Kwa mantiki hiyo Bwana Taalas, alisema kupunguza gesi chafuzi na kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi vinapaswa kuwa vipaumbele kimataifa. Viwango vya joto kwa mwaka 2018 vilikuwa kwa wastani wa nyuzi joto 0.38 katika kipimo cha selsiyasi, juu ya vipimo vya kati ya 1981 hadi 2010 vya wastani vilivyokadiriwa kuwa 14.3
Maoni
Ingia utoe maoni