Alhamisi. 21 Novemba. 2024
feature-top
Chuo Kikuu Bethlehemu bado kupata mwafaka kati ya wanafunzi na mamlaka ya chuo kutokana na kuongezeka kwa gharama za masomo

Bado hawajaweza kupata mwafaka wa matatizo ambayo yanahatarisha kushindwa kwa mwendelezo wa muhula wa kwanza wa kitaaluma katika Chuo Kikuu Katoliki cha Bethlehemu

Ni Taasisi ya Kipapa inayoendeshwa na Shirika la Ndugu wa Mashule ya Wakristo iliyoanzishwa kwenye miaka ya 70 kwa utashi wa Mtakatifu Paulo VI kama chombo cha mafunzo ya vijana wa kipalestina katika mji aliozaliwa Yesu, lakini leo hii inaishi kipindi kigumu ambacho kimesababishwa kutokuelewana kati ya mamlaka na wawakilishi wa wanafunzi, kutokana na ongezeko gharama za uendeshaji ambapo umetokana na mchango wa kiuchumi kwa upande wa wanafunzo waliojinadikisha muhula wa masomo.

Taarifa zilizo wafikia shirika la Habari za Kimisionari Fides kwa mujibu wa Makamu Rais wa Chuo kukuu  Frateli Michel Sansu anasema hata leo hii wanajadiliana na wawakilishi wa wanafunzi ili kutafuta mwafaka wa matatizo kwa kuwafanya wanafuniz warudi darasni ili kuendelea na masomo. Iwapo hilo halitafanyika Wazi ri wa Elimu wa  Palestina ametangaza kufuta muhula wa Masomo katika Chuo chao kutokana na kutofikisha idadi ya masaa ya masomo ambayo yanatoa utambulisho unaofaa katika muhula wa masomo.

Kipeo cha Chuo Kikuu Bethlehemu, kimeanza tena katika wiki hizi za mwisho. wa Chuo Kikuu alikuwa ametngaza kuachishwa kwa muda mfupi wa masomo  tarehe 6 Februari 2019, Frateli Petr Bray Makamu Kansela wa kozi za chuo kikuu katika muhula wa kwanza ambao ulianza tarehe 18 Januari, kutokana na kukatisha mara kwa mara vipindi na wawakilishi wa seneti ya wanafunzi. Wawakilishi wa wanafunzi hadi sasa wamekuwa wakizungumza na kukabiliana juu ya ongezeko la karo ya mafunzo kwa wanafuniz wa Kitivo cha uuguzi na Mafunzo ya Sayansi ili kupunguza gharama iliyoombwa ilipwe na wanafunzi.

Ongezeko la gharama ya mafunzo ulikuwa imewekwa katika mswada wa mwaka 2016.Chuo kikuu cha Bethlehemu kinasaidia nusu ya gharama zote za kozi  za wanafunzi,ka mdaada utokao kwa wafadhili wa nje. Katika barua ya hivi karibuni ilitolewa na wakuu wa chuo Kikuu, walikuwa wanathibitisha kwamba hata Chuo Kikuu katoliki kinapaswa kipewe dola milioni 1,3 kutoka kwa mamlaka ya Palestina, lakini suala hili halijatokea. Huu ni uzito juu ya hali ngumu itokanayo na kuongezeka kwa gharama za shughuli za mafunzo nje ya chuo kikuu na ile ya majengo ya Afya nchini Palestina moja kwa moja  na mabayo imetokana na kukatwa kwa fedha na msaada wa Kipalestina kutoka Marekani.

Taarifa mahali za Upatriaki wa Kilatini huko Yerusalem unasema Marekani ilikata dola za kimarekani milioni 56 ambazo ni msaada kati ya dola za kimarekani milioni  125 ambazo ziliwekwa na Umoja wa mataifa kwa ajili ya msaada wa wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) na tarehe 25 Agosti  walikata dola milioni 200 za msaada wa Mamlaka ya Palestina kwa namna ya pekee katika sekta ya afya, mafunzo na uwekezaji kwa ajili ya jamii (Fides 20/2/2019).


Maoni


Ingia utoe maoni