Jumamosi. 23 Novemba. 2024
feature-top
Kambi ya Kakuma nchini Kenya ya wakimbizi inahitaji kusaidiwa kwani kuwekeza kwa vijana wakimbizi ni kuwekeza amani endelevu

Kuwekeza kwa vijana wakimbizi walio kambini Kakuma nchini Kenya ni kuwekeza kwa amani na utulivu kwa kikanda. Hayo yamesemwa na mwakilishi wa kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa ajili ya Pembe ya Afrika, balozi Mohamed Affey.Na Mamia ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliokuwa wakiishi Sudan kwa miaka mingi sasa wameanza kurejea nyumbani kwa hiyari

Kuwekeza kwa vijana wakimbizi walio kambini Kakuma nchini Kenya ni kuwekeza kwa amani na utulivu kwa kikanda. Hayo yamesemwa na mwakilishi maalumu wa kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa ajili ya Pembe ya Afrika, balozi Mohamed Affey, baada ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Kakuma. Balozi Affey akizungumza na vijana mbalimbali wakimbizi kambini hapo, ambao asilimia kubwa ni kutoka Somalia na Sudan Kusini na baada ya kusikia maoni yao amesema kuwa anaamini uwekezaji kwa vijana hao utakuwa uwekezaji bora kwani, amefurahishwa alicho kishuhuda huko Kakuma na kwamba ni mfano wa kimataifa kwa jinsi wakimbizi na jamii za wenyeji wanavyoshirikiana, kufanya kazi pamoja na kuishi pamoja kwa utulivu.

Asilimia kubwa ya vijana hawa wakimbizi wanakabiliwa na changamoto hasa za ajira na kutimiza ndoto zao, japokuwa Balozi Affey anasema, hawajakata tamaa kwani naye amehamasika na kushuhudia matumaini waliyo nayo machoni mwa wakimbizi hao, licha ya changamoto zinazowakabili kila siku. Ametiwa moyo na wasichana aliowaona katika shule za msingi za Morneau Shappelle na Anjelina Jollie ambao anathibitisha, wanatia moyo kwamba, matumaini ya ukanda huo utadhibitiwa na jinsi wanavyowahudumia na kuwapa elimu ni ishara kwamba wakiwekeza kwa vijana hususan kwa vijana wakimbizi wanawekeza katika amani na utulivu wa kikanda. UNHCR imekuwa msitari wa mbele kwa kushirikiana na wadau wengine kuwekeza katika miradi mbalimbali itakayohakikisha vijana wakimbizi wanakuwa na matumaini ya maisha na mustakbali wao.

Hata hivyo kuhusiana na suala hili la wakimbizi hata nchini Sudan ya kusini taarifa nyingine inasema kuwa, Mkataba wa amani uliotiwa saini hivi karibuni Sudan Kusini kwamba kuna  hamasa kubwa kwa mamia ya wakimbizi wa nchi hiyo walioko Sudan kutaka kurejea nyumbani baada ya kuishi ukimbizini kwa miaka mingi.

Mamia ya wakimbizi wa Sudan Kuisini waliokuwa wakiishi Sudan kwa miaka mingi sasa wameanza kurejea nyumbani kwa hiyari. Kwa mujibu wa tarifa ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS)iliyotolewa tarehe 21 Februari 2019 inasema, takriban wakimbizi 500 wa Sudan Kusini wamewasili Bentiu baada ya kuishi ukimbizini kwa miaka kadhaa.

UNMISS inasema hatua hiyo inafuatia kutiwa saini kwa mkataba mpya wa amani miezi mitano iliyopita hatua iliyowahamasisha wakimbizi hao kurejea nyumbani kwa hiyari. Akizungumzia kuwasili kwao kamishina kanda ya Tubkona Bwana Kur Yai amesema, mabasi matano yalikuwa yamejaza wakimbizi hao ambao ni wanawake na watoto yamewasili Bentiu usiku wa kuamkia tarehe 21 Februari 2019 na mengine mengi yanatarajiwa kuwasili. Ameongeza kuwa kufutia kuwasili kwa wakimbizi hao serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba ujumuishwaji wa wakimbizi hao kwenye jamii unakuwa shwari na unaostahili.


Maoni


Ingia utoe maoni