Shirika la Saidia Watoto (Save the Children) wanasema ni zaidi ya watoto 2500 wahamiaji ambao familia zao zinashukiwa au kuwa na mahusiano halisi na magaidi na kwa sasa wanaishi katika makambi yaliyorudikana na wakimbizi kaskazini mwa nchi na kati yao ni watoto 38 wasio kuwa na msindikizwaji. Wito wa Shirika (Save the Children) linalohakikisha kuwarudisha makwao, kuwalinda na kuwashirikisha watoto na familia zao kwa misingi ya haki za kitaifa umetolewa tarehe 21 Februari 2019 kwa kuthibitisha kuwa ni zaidi ya watoto wenye asili ya mataifa 30 na kati yao watoto 38 hawana msindikizaji na wanaishi kwa sasa kati ya makambi matatu ya wakimbizi yaliyoko Kaskazini Mashariki ya Siria. Shirika la Saidia watoto (Save the Children) ambao kwa miaka 100 linajikita kupambana ili kuokoa watoto walioko hatarini na kuwahakikishia wakati endelevu,wanawaalika Jumuiya ya kimataifa kujifunga kibwebwe kwa haraka ili kuhakikisha mipango ya lazima ya ulinzi wa watoto wote.
Watoto hawa wanatoka katika familia zinazoshukiwa au halisi za magaidi.Taarifa yao inasema, watoto hawa wanatoka katika familia zinazoshukiwa au ni halisi na magaidi ambapo kwa sasa wametengwa na watu wengine katika makambi, japokuwa ni katika hatari ya kuona wananyimwa mahitaji muhimu ya lazima na huduma msingi. Sehemu kubwa ya watoto hao wanaishi na mama zao wakati watoto ambao hawana mtu wa kuwasindikizwa wanatunzwa na watu wengine waliowekwa. Katika kesi nyingine, Save the children inaeleza kuwa, watoto wasichana walikuja kutoka nchi za nje na wamelelewa na magaidi, leo hii wamekuwa wamama na wengine kuwa na watoto wa wiki chache. Pamoja na juhudi za mamlaka ya nchi ya Siria ya Kaskazini kwa kuhakikisha mahitaji ya familia, ugumu wa kipindi cha baridi ni mkali kiasi cha kuacha watu katika hali ya mahangaiko na kuwepo hatari kubwa hasa maisha ya watoto wadogo. Save the Children kwa sasa inajitahidi katika kutoa msaada katika makambi matatu kwa watu waliorundikana, lakini ni dharura kuhakikisha kutoa huduma ya watoto katika hali halisi ya ulinzi, afya na lishe, ili waweze kushinda uzoefu wa mbaya waliopitia. Na kwamba kwa sasa haiwezekani kutokana na ukosefu wa usalama Kaskazini Mashariki mwa Siria.
Naye Sonia Khush, Mkurugenzi mtendaji wa Save the Childre nchini Siria anasema Watoto wote na familia na wenye mahusiano yanayoshukiwa au kweli na magaidi ni waathirika wasio kuwa na hatia katika migogoro na lazima kufikiriwa kama jinsi ilivyo.. Mataifa yote ambayo watu wao wamejikuta wamezuiwa nchini Siria, lazima kutafuta namna ya kuwasaidia wazalendo wake. Iwapo baadhi ya Mataifa wameweza kufanya hivyo, lakini bado nchi nyingi zikiwemo hata idadi ya nchi za Ulaya ambao hawajafanya hivyo kuhakikisha usalama wa watoto na familia zao. Hii ni tabia ambayo haiwezi kueleweka iwapo unafikiria hali halisi ya hatri ya maisha yao wanayoishi huko Siria. Aidha anaongeza kusema kama ilivyojitokeza kwa mamilioni ya watoto wa Siria, hata wao wameweza kuishi nguvu za migogoro, mabomu na ukosefu wa kila aina ya mahitaji na msaad maalum ili kushinda uzoefu mbaya kwa kurudia katika hali ya kawaida na familia zao. Na sula hili lakini haliwezekani kutokea katika makambi ya wakimbizi walio rundikana na katika maeneo ambayo bado yana hatari ya kutisha katika mapambano ya kutumia silaha. Jumuiya ya kimataifa lazima ijikite sasa kabla ya kuchelewa anathibisha Sonia Khush, Mkuregenzi mtendaji wa Save the Children.
Majeshi ambayo yanathibiti magaidi, yatasabisha kwa kiasi kikubwa cha mrundikano wa watu wengine zaidi katika wiki zijazo na hivyo Save the Children inatoa wito kwa mataifa mbalimbali ili waweze kuhakikisha wanaingilia kati kwa ajili ya usalama wa wazalendo wao wambao wamo katika maeneo ya Kipeo hicho. Tangu Januari ni familia za wahamiaji 560 wakiwa na zaidi ya watoto 1.100 pamoja na maelfu ya familia za Siria waliofika katika Makambi ya wakimbiz mara baada ya kuonea chupuchuo na mapambano huko Hajin e Baghouz, na walifikia tena maelfu ya wakimbizi ambao wanaioshi kwenya makambi tangu 2017 baada ya mapambano ya Raqqa. Karibia watoto 50 wa Siria, Iraq na mataifa mengine wamepoteza maisha yao katika harakati za kukimbia mapambano hato wakikimbilia katika makambi yaliyo na mrundiko wa watu.
Watoto ambao walikuwa wanaishi katika maeneo yanayothibitiwa na magaidi walijinyimwa kila aina ya msaada wa madawa na chakula cha lazima kwa miezi kadhaa na sasa watoto hao wanaendelea kufika katika makambi hayo katika hali kweli ya kutisha na kuwawekwa katika majaribu magumu kwa wahudumu wa mfumo wa msaada wa kibinadamu. Kutokana na hilo, Shirika la Saidia Watoto (Save the children) wanaomba nchi asili waweza kuwarudisha watu wao kwa ulinzi, hasa watoto na familia zao kwa mpango maalum wa ushirikishwaji na fungamani wa haki za kimataifa.
Maoni
Ingia utoe maoni