Jumatano. 04 Desemba. 2024
feature-top
Padre Ernesto Cardenal amepata msamaha wa adhabu yake kutoka kwa Papa Francisko!

Padre Ernesto Cardenal ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni chini ya uongozi wa Rais Daniel Ortega, kwa sasa ni mgonjwa hawezi tena kitandani! Amemwomba Baba Mtakatifu Francisko ili aweze kumwonea huruma na hatimaye, kumfungulia vifungo vyote vya Sheria, Kanuni na Taratibu za Kanisa, ili aweze kumalizia maisha yake katika amani, huku akiwa Padre.

Baba Mtakatifu Francisko amemwondolea adhabu zote kadiri ya sheria, kanuni na taratibu za Kanisa, Padre Ernesto Cardenal aliyekuwa amesimamishwa kutoa huduma za Kipadre kutokana na kujihusisha sana na masuala ya kisiasa kama mwana mapinduzi nchini Nicaragua. Kwa muda wa miaka 35, hakuweza kuadhimisha Mafumbo ya Kanisa hadharani. Lakini, baadaye alitubu na kuachana na masuala ya kisiasa na kwa muda mrefu sasa amekuwa akitafakari kuhusu wito na maisha yake.

Padre Ernesto Cardenal ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni chini ya uongozi wa Rais Daniel Ortega, kwa sasa ni mgonjwa hawezi tena kitandani! Akamwomba Baba Mtakatifu Francisko ili aweze kumwonea huruma na hatimaye, kumfungulia vifungo vyote vya Sheria, Kanuni na Taratibu za Kanisa, ili aweze kumalizia maisha yake katika amani, huku akiwa Padre.

Baba Mtakatifu Francisko akiwa amejawa wingi wa huruma na upendo, kwa Padre Ernesto Cardenal aliyejuta na hatimaye akatubu udhaifu wake, tarehe 18 Februari 2019 akamfungulia vifungo vyake vyote. Padre Ernesto Cardenal ambaye kwa sasa ana miaka 94 amepewa taarifa hizi kutoka kwa Askofu mkuu Waldemar St. Sommertag, Balozi wa Vatican nchini Nicaragua, ambaye ameadhimisha Ibada ya Misa pamoja naye, Hospitalini ambako kwa sasa amelazwa kutokana na uzee na maradhi mbali mbali yanayomsumbua.

Baba Mtakatifu anamwombea Padre Ernesto Cardenal neema na baraka, ili aweze kuishi kwa amani na utulivu, huku akiendelea kumtafakari Kristo Yesu, Ufunuo wa huruma na upendo wa Baba wa milele. Kwa upande wake pia, Padre Ernesto Cardenal amemshukuru Baba Mtakatifu pamoja na Askofu mkuu Waldemar St. Sommertag, Balozi wa Vatican nchini Nicaragua kwa juhudi zake. Padre Ernesto Cardenal enzi za ujana wake, alikuwa ni mwanataalimungu mahiri nchini Nicaragua. Akajipambua katika kupambana na ujinga na kuwawezesha wananchi wengi wa Nicaragua kujua kusoma na kuandika. Sasa anataka kupumzika kwa amani, akiwa kama Padre, baada ya kupiga vita na hatimaye, kuilinda imani yake!


Maoni


Ingia utoe maoni