Jumatano. 04 Desemba. 2024
feature-top
Papa Francisko anatarajiwa kutembelea Makao Makuu ya Jiji la Roma, Campidoglio, tarehe 26 Machi 2019

Baba Mtakatifu Francisko amekubali mwaliko kutoka kwa viongozi wa Jiji la Roma, uliotolewa na Meya wa Jiji, Virginia Raggi ambaye amekuwepo madarakani kuanzia tarehe 22 Juni 2016. Baba Mtakatifu anatarajiwa kukutana na Baraza la Ushauri la Jiji la Roma, hapo tarehe 26 Machi 2019.

Baraza la Makardinali Washauri, katika Kikao chake cha XXVII liliwasilisha Muswada wa Katiba mpya ya Kitume inayojulikana kama “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili. Makardinali wakapembua kazi yao katika kipindi cha miaka mitano; wakaangalia muundo wake kwa kuzingatia kwamba, baadhi ya Makardinali umri unazidi kwenda mbio na kadiri ya sheria, kanuni na taratibu za Kanisa wanapaswa kung’atuka kutoka madarakani.

Makardinali walidadavua pia mkutano wa Marais wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki duniani pamoja na Baba Mtakatifu Francisko; changamoto kwa Kanisa kusimama kidete kulinda watoto wadogo dhidi ya nyanyaso za kijinsia, kashfa ambazo zimechafua maisha na utume wa Kanisa katika ulimwengu mamboleo! Walipitia kwa mara nyingine tena utekelezaji wa mageuzi kwenye Baraza la Kipapa la Mawasiliano kadiri ya Barua binafsi kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko ya mwaka 2015, inayotaka kuunganisha: Radio, Televisheni na Gazeti la L’Osservatore.

Lengo kuu la Baba Mtakatifu ni kuongeza tija na kuleta ufanisi katika huduma kwa kuunganisha vyombo vya mawasiliano vya Vatican ambavyo vina utajiri mkubwa wa watu kutoka katika tamaduni na lugha. Professa Vinvenzo Bonomo, Gombera wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano na mjumbe wa Serikali ya Vatican, amegusia sheria, taratibu na kanuni mpya za mji utawala wa mji wa Vatican zilizoridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 7 Desemba 2018.

Baba Mtakatifu Francisko amekubali mwaliko kutoka kwa viongozi wa Jiji la Roma, uliotolewa na Meya wa Jiji, Virginia Raggi ambaye amekuwepo madarakani kuanzia tarehe 22 Juni 2016. Baba Mtakatifu anatarajiwa kukutana na Baraza la Ushauri la Jiji la Roma, hapo tarehe 26 Machi 2019. Itakumbukwa kwamba, Papa Francisko na Waziri mkuu wa Italia Bwana Giuseppe Conte walikutana na kufanya mazungumzo ya faragha kunako tarehe 15 Desemba 2018. Viongozi hawa walijafdili pamoja na mambo mengine kuhusu: athari za mabadiliko ya tabianchi; huduma ya ukarimu na upendo kwa wakimbizi na wahamiaji mintarafu Mkataba wa Kimataifa wa Usalama wa Wahamiaji wa mwaka 2018 pamoja na Mkutano 24 wa Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP 24 Katowice, pamoja na umuhimu wa kulinda na kudumisha amani duniani.



Maoni


Ingia utoe maoni