Jumatano. 04 Desemba. 2024
feature-top
Maprofesa na wanafunzi wa Taasisi ya Augustinianum tarehe 16 Februari 2019

Baba Mtakatifu Francisko katika mkutano na Taasisi ya Kitivo cha Mababa wa Kanisa katika fursa ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake,amewashauri maprofesa kuwa waaminifu wa jukumu la kuandaa wanafunzi washiriki maisha ya Kanisa na mijadala juu ya changamoto za dunia ya sasa

Ninayo furaha ya kuwakaribisheni katika fursa ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Mafunzo ya Mababa wa Kanisa “Augustinianum”. Ninamshukuru Padre Alejandro Moral Antón, Mkuu wa Shirika la Wagositiano na Gombera wa Taasisi. Aidha Rais wa Taasisi hiyo, Padre Giuseppe Caruso washauri, wahudumu na wajumbe wote wa kitivo pamoja na wanafunzi wote. Kwa nama ya pekee mmoja wa ndugu yenu ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Taasisis hiyo, Kardinali Prosper Crech. Ninapenda pia kuwasalimia maprofesa wastaafu waliopo, lakini ambao wameacha mfano hai katika Taasisi. Ninamkumbuka Profesa Maria Grazia Mara,ambaye alifundisha mambo mengi na sasa ana miaka 95 lakini bado anaendelea kutangaza na kufundisha katisimu kwa watoto. Hata Kardinali Grech: mahubiri yake ni rahisi … yenye hekima kwa maana unapofikia umri kama huo ni kugeuka kuwa na urahisi mkubwa ambao unafanya mambo mema. Ninawashukuru sana wazee na maprofesa wastaafu. Ninaungana nanyi katika furaha hii ya kushirikishana jubilei pamoja.

Shukrani kwa waanzilishi wa mafunzo ya mababa wa Kanisa

Ndiyo mwanzo wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 16 Februari 2019 alipokutana na wajumbe wa Taasisi ya Kipapa ya Agostianianum,wakiwa katika fursa ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake kunako tarehe 14 Februari 1969. Baba Mtakatitifu akiendela anasema hii ina maana hawali ya yote kumshukuru Mungu kwa kile ambacho wagositiani wamewezesha kutimiza kwa kipindi cha nusu karne. Lakini wakati huu  unatoa mwaliko wa kufikiria kumbukumbu na kupongeza hatua zote kufikia asili ya kukumbuka alichoeleza Mkuu wa shirika kwenyehotuba yake katika mantiki ya wingi wa utamaduni wa shirika la Wagostiani ambao walianzisha mjini Roma mafunzo yanayojikita katika sayansi takatifu kwa namna ya pekee ya  Mababa wa Kanisa na zaidi, Mtakatifu Agostino na urithi wake.

Historia ya shule ya wagostiani inajikitika katika utafiti wa hekima. Agostinianum ilianziwa kwa ajili ya kuchngia kuhifadhi na kueneza utajiri wa utamaduni katoliki hasa katika utamaduni wa Mababa wa Kanisa. Suala hili ni muhimu kwa ajili ya Kanisa. Na mtindo umekuwa hivyo japokuwa katika nyakati hizi kama alivyothibitisha Matakatifu Paulo VI wakati wa hotuba yake ya kuanzishwa kwa Taasisi kwamba: Kurudi kwa Mababa wa Kanisa ni sehemu ya kukumbusha asili ya kikristo, bila hiyo isingewezekana kupyaisha biblia, kuunda liturujia na utafiti mpya wa kutaalimungu ambao ulianzishwa na Mtaguso wa II wa  Vatican II (hotuba tarehe  4 Mei 1970). Na Mtakatifu Yohane Paulo akitembelea Taasisi hiyo kunako mwaka 1983 alisistiza akisema kujiweka katika shule ya mababa, ina maana ya kujifunza kujua vema Kristo na kujua vema mtu, na kwamba utambuzi huo unasaidia Kanisa kwa kiasi kikubwa katika utume wake (tarehe 7 Mei 1982).

 

Kutiwa moyo ili wawe waaminifu katika mzizi na kazi yao

Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo wa kuwa waaminifu katika mizizi yao na kazi yao na ili kuhifadhi wajibu wa kutangaza thamani za kiakili, kitasaufi na kimaadili ambazo zinaweza kuwaandaa wanafunzi wao washiriki kwa hekima na uwajibikaji katika maisha ya Kanisa na mijadala juu ya changamoto za nyakati zetu. Huduma hiyo inaendana sambamba na uinjilishji na kuchangia kuhamasisha ukuaji wa familia ya binadamu kuelekea katika ukamilifu wa Mungu (Cost. ap. Veritatis gaudium, 1). Hivi karibuni katika hati ya kitume ya Veritatis gaudium Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kusema, inaanza na maneno haya: Moyo wa mtu hauwezi kutulia na  kujieleza furaha ya ukweli hadi itakapokutana na kuishi kwa kushirikisha kwa wote nuru ya Mungu (VG 1 ). Ni wazi kwamba katika mwangwi wa Mtakatifu Agostino ( Rej Conf., X, 23.33; I,1,1) kwa hakika yeye alijua na kujielezea kwa hali ya juu ule utupu wa moyo wa binadamu hadi anapopumzika kwa Mungu na ambaye katika Yesu Kristo, anatuonesha kwa kina ukweli juu ya maisha yetu na juu ya hatima yetu.

Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko ameshirikishana nao maelezo ya Matakatifu Agostino yanayohusu Mafundisho ya kikristo (De doctrina cristiana) kwamba: Wale wote ambao watatangaza mambo waliyo yapta kwa wengine wasali kabla ya kupokea, kwa wale ambao watapokea na ili waweze kupewa kile ambacho wanatamani kupokea, na baada ya kupokea wasali ili nao waweze kutangaza vema na kwa ajili ya wale ambao wamepata wema waweze kutangaza na kupokea  (IV, 30, 63). Katika kuadhimisha jubilei hoyo, Baba Mtakatifu anasema wana uhakika kuwa anasali kwa ajili yao. Anawashauri hata wao kuombeana mmoja na mwingine ili Bwana aweze kuwasaidia katika jitihada zao za kila siku za utafiti, mafunzo, jumuiya ya Taasisi na wapendwa wao kwa maombezi ya Mtakatifu Agostino na Mtakatifu Monica. Amewabariki kwa Baraka Takatifu.

Kumbuka: chuo cha mafunzo ya mababa wa Kanisa kinatimiza miaka 50

Ilikuwa tarehe 4 Mei 1970 Mtakatitu Paulo VI alizindua Taasisi ya Kipapa ya Agostiano hatua chache kutoka katika nguzo za uwanja wa Mtakatifu Petro hasa  katika hattua za kitivo kipya karibu na chuo Kikuu vha Latenaneno, kilichofikiriwa kuwa na masomo ya Mababa wa Kanisa, ambao walishuhudia imani katika karne za kwanza na waatalimungu walioangazwa na kuonesha, na ambao waliweza kulinda dogma katoliki. Na katika  sehemu kubwa ya wenye shauku ya kichungaji, walihubiri kwa wote kwamba kuna mahitaji kiroho. Mtakatifu Paulo VI alipendelea kwa nguvu zote awepo Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino Padre Agostino Trape, pamoja na ndugu yake Padre Prospet Grech leo hii ni Kardinali na hiyvo  tarehe 14 Februari 1969 taasisi hiyo ilifunguliwa  na Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki waliiinua kisheria taasisi hiyo na hati ya tarehe 25 Julai.


Maoni


Ingia utoe maoni