Alhamisi. 21 Novemba. 2024
feature-top
Baba Mtakatifu Francisko akihutubia katika mkutano wa IFAD mjini Roma tarehe 14 Februari 2019

Katika makao ya Fao mjini Roma, Baba Mtakatifu Francisko ameudhuria sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa 42 wa Shirika la Kimataifa la ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD unaoongozwa na mada ya ubunifu na kuanzishwa kwa ujasiliamali katika dunia ya vijiji

Nimefikiria kuzungumza kisipanyola moja ya lugha maalum inayotumika, lakini napendelea kutumia kitaliano kwa sababu ya uhakika kwamba itakuwa bora kwa wote. Ninamshukuru Rais wa IFAD kwa maneno yake na ninafurahi sana kukutana nanyi ambao mnafanya kazi kila siku katika taasisi hii muhimu ya umoja wa Mataifa. Mnayo shauku katika kutoa haduma ya masikini wa ardhi hii, ambao kwa sehemu kubwa wanaishi katika maeneo ya vijiji na mikoa ya mbali na miji na mara nyingi katika hali ngumu ya kutia huruma. Kwa wote mlio hapa kama vile wenzenu ambao hawakupata fursa ya kufika ninawapa salam kindugu. Ndiyo mwanzo wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 14 Februari 2019, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 42 wa Shirika la Kimataifa la ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD unaoongozwa na mada ya ubunifu na kuanzishwa kwa ujasiliamali. Ni mkutano wa siku mbili unaofanyika katika makao ya FAO mjini Roma.

Neno la kwanza ni “asante”

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake amesema kwa kuifikiria wao inamjia akilini kwa urahisi maneno kadhaa,la kwanza linatoka ndani ya moyo nalo ni “asante”. Anamshukuru Mungu kwa ajili ya huduma ya kazi yao ya sababu kubwa ambayo ni ya mapambano dhidi ya njaa na taabu za dunia. Asante kwa sababu wanakwenda kinyume na dunia hii. Tabia ya sasa. leo hii inatazama kupungu kwa umaskini wa kikithiri taratibu sana na kuongeza kwa utajiri uliopo mikononi mwa wachache tu. Walio wachache wana mengi na walio wengi wanacho kidogo sana Baba Mtakatifu anathibitisha na kwamba, wengi hawana na wanaelea, wakati huo hu walio wachache wana mambo ya ziada. Hali hii ya ukosefu wa usawa ni janga kwa ajili ya wakati endelevu wa binadamu, Baba Mtakatifu anakazia na kwa maana hiyo anawashukuru sana kwa sababu ya wao kufikiria na kutenda kinyume na dunia hii. Kwa ajili ya kazi yao ya ukimya na mara nyingi imefichika, kama mzizi chini ya ardhi usioonekana, lakini utunatoa kiini cha kulisha mmea. Labda hawatambuliwi lakini anawathibitishia kwamba, Mungu anaona kila kitu, anaona kujitoa kwao na taaluma na stadi zao, anawapongeza masaa ambayo wanapitia wamekaa ofisini na sadaka ya masaa hayo. Mungu hawezi kusahau kamwe wema na anajua kumjalia aliye mwema na mkarimu.

Katika Kazi yao, inaoneakana faida kwa watu wenye kuhitaji na wasio na bahati ambao wanaishi kwa mateso makubwa katika pembezoni mwa jamii anasema Baba Mtakatifu Francisko. Ili kuweza kufanya vema  katika aina ya huduma hiyo, ni lazima kuunganisha uwezo wa namna ya kipekee wa hisia ya kibinadamu. Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu amewashauri wajikite daima katika maisha ya kiundani na hisia ambazo zinapanua moyo na kuwezesha wema wa mtu na watu. Hizi ni tunu ambazo ni zaidi ya wema wa zana anabainisha Baba Mtakatifu. Anawashukuru hata msaada wao ambao unaweza kutimiza mipango ambayo inasaidia watoto wenye shida, wanawake , na familia nzima. Mipango mizuri inayoanzishwa inapelekwa mbele kwa msaada wao. Anazidi kuwashukuru kwa kazi hiyo na kwa niaba ya maskini wengi ambao wanawahudumia!

Neno la pili ni “mbele”

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake ametoa neno la pili ambalo amependelea kuwambia ni mbele. Hii ina maana ya kufuata ubunifu katika shughuli za huduma yao, bila kuchoka, bila kupoteza matumaini, bila kukata tamaa kwa kufikifikira kuwa ni tone moja tu linaloangukia  baharini. Siri yake ni kuendelea kulinda na kuongeza shauku ya sababu zilizo za juu. Katika muundo huo, ni kushinda hatari za ugumu, unafiki na ukawaida  kwa kujikita kwa shauku kubwa kile ambacho kinafanyika kila siku hata katika mambo yaliyo madogo. Neno shauku ni zuri sana na tunaweza kutambua kama vile kumwona Mungu katika kila chochote  kinachofanyika. Hiyo ni kwa sababu Mungu hachoki kamwe kutenda wema, hachoko kamwe kuanza upya na hachoki kwamwe kutoa matumaini. Yeye ni ufunguo wa kutoweza kuchoka. Na katika kusali inasaidia kuongeza beteli nguvu safi. Anayetenda wema anaomba Bwana anayefanya kazi kandoni mwetu. Na zaidi kila hati ambayo wanajikita kukuabiliana nayo, Baba Mtakatifu anawashauri wajaribu kutafuta nyusoz. Sura za watu ambo wako nyuma ya ramani zile. Kujiweka kwa dhati ndani ya maisha yao ili kuelewa vema hali zao… Ni muhimu ili kuepuka kubaki kijujuu tu, bali kutafuta  namna ya kuingia katika uhalisia wa maisha yao na ambamo wanataka kuona sura hizi, hadi kufikia moyo wa mtu. Kwa kufanya hivyo kazi inakuwa kwa dhati kwa moyo wa wengine, matukio na historia za wote

Roho inayotembea katika "upendo" haipati shida na wengine, wala kuchoka

Jambo la mwisho Baba Mtakatifu Francisko amesema tukumbuke kile ambacho Mtakatifu Yohane wa Msalaba alisema  “roho inayotembea katika upendo haina shida na wengine, na wala kuchoka yenyewe” (maneno ya upendo na mwanga96). Ili kuweza kwenda mbele kuna haja ya kupenda. Swali la kujiuliza si kwa jinsi gani upo uzito  wa mambo ambayo ninapaswa kufanya, kinyume chake ni kujiuliza kwa ni upendo upi  ninaweka katika masaa yangu ya kazi? Anayependa ana ubunifu wa kugundua suluhisho la mahali ambamo wengine wanaona matatizo. Anayependa anasaidia mwingine kwa mujibu wa matatizo yake na kwa ubunifu, lakini si kwa mujibu wa mawazo yaliyokusudiwa au mahali pa upamoja. Shauku, kutafuta nyusso na kupenda ndiyo vitu msingi ambavyo vinaweza kusaidia kwenda mbele na kwa maaana hiyo  Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo hata wao waendelee mbele kila siku. Amehitimisha kwa kuwabariki wote, wapendwa wao na kazi wanayojikita katika IFAD kwa manufaa ya wengine ili kupambana na janga kubwa ambalo ni njaa duniani. Anawaomba wasisahu kusali kwa ajili yake au ili Mungu amjalie kuwa na mawazo mazuri.


Maoni


Ingia utoe maoni