Mbele yetu kuna jamii yenye uwezo wa kuendelea katika wema
Hali halisi hizi Baba Mtakatifu asisitiza zinaonekana katika kipindi na kwa upande mwingine jamii zetu zimeweza kupata matokeo makubwa katika mantiki ya ufahamu. Hii ina maana kwamba mbele yetu kuna jamii yenye uwezo wa kuendelea kutoa mapendekezo ya wema; na itashinda hata kwa mapambano dhidi ya njaa na umasikini wa kukithiri. Kuwa na uamuzi wa dhati katika kupambana ndiyo msingi ili kuweza kusikiliza kwa dhati kilio na kusema hapatakuwapo na njaa kwa wakati ujao, bali ilikuwa ni wakati uliopita. Lakini ili kufikia hatua hiyo ni lazima kuwapo msaada wa jumuiya ya kimataifa , jumuiya mahali ya raia na wote ambao wanamiliki rasilimali. Wahusika wa wasivamiwe kwa kupitiwa mmoja baada ya mwingine badala yake wachukue wajibu wa kupata suluhisho la dhati na halisi Baba Mtakatifu ameonya.
Uwajibu wa Vatican na mashirika yanayojikita katika maendeleo ya watu
Baba Mtakatifu anasema, Vatican imekuwa daima ikiwatia moyo juhudi zilizofanywa na Shirika la kimataia kwa ajili ya kukabiliana na umasikini. Kwani hatuwezi kusahau hata Mtakatifu Paulo VI kunako mwaka 1964 alitoa wito mkubwa duniani mjini Bombay India, pia kwa kupendekeza kwa upya katika matukio tofauti ya kuweza kuunda mfuko ambao unawezesha binadamu kumwamasisha andokane na mambo yote yanayomletea umasikini (Hotuba katika Mkutano wa dunia wa vyakula 9 hata yeye hawajasita kamwe kuhamaisha kunzishwa kwa mambo hayo na moja ya hatua hiyo inayoonekana ni IFAD yenyewe. Mkutano wa 42 wa IFAD unaoendelea katika mantiki hii na mbele yake unayo kazi ya ya kushangaza na ngumu katika kuunda uwezekano wa haraka, il kuondoa kila aina ya wasiwasi na kuwaweka kila watu katika hali zao wakabiliana na mahitaji ambayo yanawasumbua. Jumuiya ya Kitaifa ambayo inaendeleza ajenda ya maendeleo endelevu ifikapo 2030 inapaswa kutimiza hatua za kufuata na za kweli katika malengo 17 waliyojiwekea. Katika pendekezo hilo, Baba Mtakatifu Francisko anasema, msaada wa IFAD unaonesha hatua ya kuweza kufuatilia kwenye malengo mawili ya kwanza ya ajenda, ikiwa ni kusitisha umasikini na mapambano dhidi ya njaa, na pia kuhamaisha uzalishaji.
Hakuna litakalo wezekana bila kuwa na maendeleo vijijini
Hakuna lolote litakalo wezekana iwapo hapatakuwapo na maendeleo vijijini, Baba Mtakatifu amebainisha na kwamba, ni maendeleo ambayo yamezungumzwa kwa kipindi kirefu, lakini hata leo hii haya jatimizwa. Badala yeke ni kuona matokeo ambayo siyo mema kwa upande wa zaidi ya milioni 820 ya watu ambao wanateseka na chakula, utapia mlo duniani na whao wota wanaishi katika maeneo ya vijiji,na ambao wanajikita katika uzalishaji na wakati huo ni wakulima. Na zaidi wimbi la uhamiaji kutoka vijiji kwenda mijini ni suala la dunia nzima ambalo haliwezi kudharauliwa anasema Baba Mtakatifu! Maendeleo ya maeneo mahalia kwa dhati yana thamani kubwa japokuwa hayafanyi kazi kwa lengo linalokusudiwa. Hii ina maana ya kila mmoja, kila jumuiya inaweza kabisa kwa uwezo wake na kwa namna yake kwa kuishi maisha ya kibinadamu yenya hadhi na kuitwa jina kwa njia ya ushirikiano. Kwa maaana hiyo Baba Mtakatifu anatoa wito kwa wote wenye majukumu ya kimataifa na mashirika yasiyo kuwa ya kisekiliaka kama vile kwa wote wadau wanaojikita kuchangia katika sekta ya umma na binafsi,ili kuendeleza mikondo ya lazima katika kujikita kwenye matendo kwa kiwango kinachostahili katika kanda za vijiji duniani ili wote waweze kuwa wasanii na wahusika wa uzalishaji kwa ajili ya maendeleo.
Ubunifu na teknolojia vijijini iendane na utamaduni
Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari kwao inayotazama mada inayoongoza mkutano huo wa IFAD ambayo ni ubunifu na kuanzishwa kwa ujasiliamali katika dunia ya vijiji. Inabidi kuchuchumalia ubunifu, juu ya uwezo wa wajasiliamali na wadau wote wa sekta mahalia na upatikanaji wa mchakato wa uzalishaji kwa sababu ya kuweza kupata mabadiliko ya vijiji, na hatimaye kuweza kusitisha utapiamlo na kuendeleza kwa namna ya ubunifu wa mantiki ya kilimo. Katika mantiki hiyo ni lazima kuhamasisha sayansi na dhamiri na kuweka teknolokoa ya kweli katika huduma kwa masikini. Mengineyo, teknolojia mpya haiwezi kutofungamana na utamaduni mahalia, kuwa na utambuzi wa tamaduni, lakini pia ni kufungamanisha na kutana kwa njia ya mkakati wa pamoja. Anawatia moyo wote washiki wa Mkutano huo na wale ambao wanajikita katika Shirika hili la IFAD kwa kazi yao na wasiwasi wao ambao uweze kweli kuleta manufaa kwa wale ambao wamebaguliwa , ni waathirika wa sintofahamu na ubinafsi na kwamba inawezakana kuona kuona mapambano ya dhati yanafanyika ya kusitisha njiia na kuwa na haki na ustawi kwa wote.
Maoni
Ingia utoe maoni