IFAD ni Shirika la kimataifa la ufadhili wa maendeleo ya kilimo, ambalo ni shirika la Umoja wa mataifa kwa ajili ya maendeleo vijijini lilioanzishwa tarehe 13 Desemba 1977 kwa lengo kufanya ukue uzalishaji wa kilimo na vyakula haki kufikia kwa ngazi ya maisha ya kujitosheleza. Kwa namna hiyo unafadhili wa mipango ya kimaendeleo na ambayo ni muhimu kwa masikini zaidi kati ya masikini duniani na ambao wanaishi katika vijijini pembezoni kabisa mwa miji. Ni 70% ya watu duniani mara nyingi wamesahuliwa na wenye kuhitaji msaada mkubwa. Ufuatiliaji wa Vatican katika Shirika ka Ifad umekuwapo tangu mwanzo. Kwani hatuwezi kusahau hata Mtakatifu Paulo VI kunako mwaka 1964 alitoa wito mkubwa duniani wa kuweza kuunda mfuko na uwezekano ambao unawezesha binadamu katika mambo ya chakula na kujikita kwa ajili ya maskini duniani, kufadhili mipango ya kuwazesha huduma ya vifaa kama vile mbegu na zana, mbolea, mipango ya umwagiliaji na maghala ya kuwekea nafaka na majengo katika maeneo ya vijiji. Kwa njia hiyo Vatican inafuatilia kwa kina suala hili kwa sababu inatambua umuhimu wa kusaidia maskini wa ardhi hii. Hilo ndilo lengo la mwisho kwa haki ya watu, vyama na kama heshima ya ardhi ambayo ndiyo mada kuu pendevu kwa Baba Mtakatifu Francisko.
Katika kuelekea kwanye Mkutano wa Ifad tarehe 14 Februari 2019
Vatican News imefanya mahojiano na Monsinyo Fernando Chica Arellano, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Makao ya Fao, Ifad na Pam mjini Roma kuhusu mambo ambayo yatakuwa katika kiini cha Mkutano wa IFAD na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 14 Februari 2019. Anasema kwamba ni mada ambazo daima amekuwa akipeleka mbele tangu akiwa kijana. Pia hatupaswi kisahau asubuhi mapema kwenye mkutano huo wa Ifada Baba Mtakatifu Francisko pia atakutana na watu wa asilia kwa sababu ni sambamba na maadhimisho ya Mkutano wa IV wa Muungano wa Jukwaa za watu wa asili duniani ulioitishwa na IFAD yenyewe. Mwezi Oktoba mwaka huu itafanyika Sinodi ya Amazoni, kwa maana hiyo mada hizi zinaingiliana sana na mawazo ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye daima yuko karibu na masikini wa ardhi hii.
Ratiba ya Mkutano wa IFAD tarehe 14-15 Februari
Katika mpango wa shughuli ya mkutano wa tarehe 14-15 Februari 2019 ambao ni maalum kwa namna ya pekee kuna kuonesha nafasi ya vijana katika kuhamasisha kazi za vijana mwenye maendeleo ya vijiji ili vijana wawe ni mizizi ya maeneo yao na kuepuka kukimbia ameneno yao, Monsinyo Arellano anathibitisha kuwa maeneo ya vijiji daima yanageuka kuwa jangwa la vijana ambamo vijana wengi wanahama wakijaribu kutafuta wakati endelevu wa maisha yao lakini mara nyingi.Kwa maana hiyo kuna umuhimu wa kuwekeza katika vijana na kuwapa uwezekano wa kiteknolojia, na katika kuwekeza amani. Kuwekeza vijana katika ufundi kwa sababu leo hii Kilimo ni karibu sana na mambo yote ya ubunifu ambayo yanawezesha kuchanua kwa ardhi kwa namna ya dhati hai na hasa uendelevu.
Aidha akielezea juu ya hali halisi ya ushirikiano katika mtazamo wa IFAD kufikia hatua ya kuunda mipango ya dhati, anasema ili kuuendeleza ushirikiano na katika mipango ya kufadhili ni moja ya lengo la Ifad. Ushirikiano lazima uwe ndiyo ufunguo wa kufikiria maendeleo. Kusema ushirikiano maana yake ni kusema mshikamano na bila mshikamano hakuna maendeleo yanayowezekana. Suala hili ndilo hata moyo wa Baba Mtakatifu Francisko ya kwamba mshikamano ni kama injini ya maendeleo. Kwa dhati ni upendo wa kijamii na bila upendo dunia hii haiwezi kutembea kwa sababu kitakachookoa dunia hii ni upendo na siyo fedha bali upendo tu.
Baba Mtakatifu alitembelea hata Fao 2017
Kwa hakika pia tukumbuke ziara ya Papa katika makao ya Fao Oktoba 2017, Baba Mtakatifu katika hotuba yake aliomba kuanzishwa kwa lugha ya ushirikiano kwa maana ya upendo unaojikita katika kutoa bure, mshikamano wa utamaduni wa zawadi na hivyo, Monsinyo anaongeza kuthibitisha kuwa alitoa ujumbe huo kwa sababu upendo ni ukamilifu wa ubinadamu, kwa hakika maneno yake yalikuwa yanasubiriwa kwa sababu mazungumzo ya kimataifa hayawezi kukua, kile kinachokuwa ni sintofahamu. Wanapozungumza juu ya ujasiriamali, lazima kuzungumza maendeleo ambayo ni mema na yenye kusimika mizizi ndani ya eneo mahalia. Hiyo ni kwa sababu anasema, maendeleo yanatokea katika hali iliyo na mpangilio na ushiriki kwa wote. Kuzungumza juu ya ujasiliamali maana yake ni kuzungumza kwa dhati nguvu, mawazo, mantiki za mkakati na utaratibu. Huo ndiyo ujasiliamali wa kweli na ambao kweli unahitahiji nguvu zaidi na kwa pamoja katika dunia ya leo.
Maoni
Ingia utoe maoni